HALMASHAURI YA MANISPAA BUKOBA INAWATANGAZIA WANANCHI UUZAJI WA VIWANJA 5,000 VILIVYOPIMWA..MAWASILIANO +255754 623938 Email :crwegasira2001@yahoo.com
Maeneo yaliyopimwa viwanja na idadi ya viwanja vilivyopo
Na | Eneo/mahali | Idadi ya viwanja [Makadirio] |
1 | Buhembe | 1161 |
2 | Kyasha | 750 |
3 | Mugeza | 460 |
4 | Rwazi | 348 |
5 | Rwome | 202 |
6 | Ijuganyondo | 117 |
7 | Ihungo | 364 |
8 | Makongo | 216 |
9 | Nshambya | 296 |
10 | Kagondo Kaluguru | 504 |
11 | Nyanga | 505 |
(c) Maelezo ya Fedha ya dhamana.
Na | Aina ya Mwombaji | Fedha ya dhamana kwa kila kiwanja |
1 | Mwombaji Binafsi | 200,000.00 |
2 | Taasisi kama Mashirika, Benki, Taasisi za dini, Shule, Mifuko ya Hifadhi ya jamii n.k | 500,000.00 |
NB: Kwa waombaji ambao wataomba viwanja zaidi ya tisa (kwa kutumia fomu Namba 2) watatakiwa kulipia fedha ya dhamana ya Tshs: 500,000.00 kwa kila kiwanja.
MAELEZO KWA WAOMBAJI.
1. Uuzaji wa fomu za maombi viwanja katika Manispaa ya Bukoba utaaza tarehe 23 Aprili 2012 hadi tarehe 22 Mei, 2012.
2. Bei ya Kununua fomu hii ni Tsh. 10,000/= (Fomu zinapatikana Benki ya Posta – Tawi la Bukoba).
3. Tafadhali rejesha fomu iliyojazwa vizuri katika Benki ya Posta – Tawi la Bukoba na utapewa fomu ya uthibitisho.
4. Tafadhali jaza fomu tofauti kwa kila kiwanja (fomu Namba 1) ikiwa unaomba kati ya viwanja viwili hadi 9 (viwanja chini ya 10).
5. Kama utapendelea kuomba viwanja vingi (kuanzia 10 na kuendelea),
tafadhali tumia fomu namba 2 (inapatikana Benki ya Posta – Tawi la Bukoba).
6. Ukubwa wa viwanja: (a) Ujazo mkubwa-High density (400-800) mita za eneo; (b) Ujazo wa kati-Medium density (801 -1200) mita za eneo; na (c) Ujazo mdogo-Low density (1201 - 4000) mita za eneo
7. Dhamana itarejeshwa kupitia benki ya Posta ikitokea haujafanikiwa kupata kiwanja
8. Kwa maelezo zaidi/ufafanuzi wa yote hapo juu, tafadhali wasiliana na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba.