HAPA NA PALE NA CAMERA YETU
Kabla sijajua kisa cha valangati hili kwanza ni kucheza na Camera...
Kisa ni kwamba kijana mmoja "mtanashati" aliyejichanganya mtaa wa Wamachinga waliopo barabara ya Government mkabala na msikiti wa Jamia.
Alionekana akitokea Nyuma ya Vibanda vya machinga hao,ndipo machale yalipowacheza na ikatokea hali ya sintofahamu na kuanza kumhoji ni wapi anatokea na baada ya kijana huyo kukosa jibu sahihi ndipo akatembezewa kichapo kikali kutoka kwa Machinga hao.