KAMPUNI YA LG YAJA NA KIYOYOZI KIPYA AINA YA MULTI-V 3
Mkrugenzi wa kampuni ya LG kwa upande wa Tanzania akiongea na wageni waalikwa waliofika katika uzinduzi wa Kinyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3, vinavyosambazwa na kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Fundi mkuu wa Kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wasambazaji wa kiyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3 Bw. Emmanuel Myollah akiwahakikishia ubora wa viyoyozi hivyo wageni waliofika katika uzinduzi huo.
Fundi mkuu wa Kampuni ya Alshaaf ambao ndiyo wasambazaji wa kiyoyozi kipya aina ya MULTI-V 3 Bw. Emmanuel Myollah akiwahakikishia ubora wa viyoyozi hivyo wageni waliofika katika uzinduzi huo.
Msajili Msaidizi wa bodi ya wahandisi nchini engineer Fares Washa akitoa machache katika uzinduzi guo.
Msajili wa bodi ya wahandisi nchini engineer Steven Mlote akitoa machache katika uzinduzi huo. Ambapo aliwashukuru kampuni ya LG kwa kuleta teknolojia mpya ya viyoyozi aina ya MULTI-V 3 na vyenye ubora wa uhakikaWarembo wakifungua kwa taratibu pazia zilizokuwa zimefunika kiyoyozi huo ili kuashiria uzinduzi.
Wakurugenzi wa kampunya LG na Wahandishi wa bodi ya Wahandisi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi.
Wageni wakibadilisha mawazo katika uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Baadhi ya waandishi wa Habari kutoka vyombo mbali mbali waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini.
Tanzania imechaguliwa kuwa moja kati ya nchi pekee chache barani Afrika ambapo LG imeamua kuzindua viyoyozi aina ya MULTI-V 3, ambazo ni toleo la tatu (tabaka la tatu) la aina ya viyoyozi aina ya VRF Air Conditioning bora kwa matumizi ya majengo ya biashara na makazi ya saizi ya kati.
Viyoyozi vya Multi- V 3 vinafaida tatu kwa kuu kwa watumiaji ikiwemo ufanisiwa hali ya juu, uwezo mkubwa zaidi na faida ya kuwa na bomba refu.
Kampuni la LG linalenga kubuni na kukuza bidhaa zinazotumia nishati kwa ufanisi, natamka kwa kujivuna kwamba bidhaa hii itakidhi matakwa bora ya wateja pamoja usalama wa bidhaa kutokana na teknolojia ya udhibiti umeme na zaidi kutokana na faida za utunzaji wa mazingira kwa viwango vya kisasa.
Alshaaf ndio wakala pekee rasmi wa kusambaza na kufunga bidhaa za viyoyozi vya LG hapa Tanzania, naamini kwamba nchi yetu itaongoza katika kulinda viwango vya kimataifa vya utunzaji wa tabaka la hewa na utunzaji mazingira. Katika kipindi hiki cha mtikisiko wa upatikanaji nishati duniani, bidhaa za LG zimeundwa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa zinazolinda matumizi ya ziada ya nishati.
Tunawapongeza washirika, LG na Alshaaf kwa jitihada zao endelevu za kutoa huduma za ueledi za viyoyozi Tanzania kwa miaka 25 sasa na kujenga njia inayoruhusu LG kuwa imara Tanzania kama wakala wao rasmi.