MHE. MASSAWE AKEMEA VYAMA VYA USHIRIKA KUTOJIHUSISHA NA KESI MKOANI KAGERA BADALA YAKE VIBORESHA MAISHA YA WAKULIA
Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe akemea vyama vya ushirika mkoani Kagera kujihusisha na kesi mbalimbali zinazoweza kuvizoofisha vyama hivyo na fedha za wanachama ambao wengi wao ni wakulima kutumika kuendesha kesi hizo mahakamani.
Mheshimiwa Massawe ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Ushirika mkoani Kagera (Kagera Co operaatve Union 1990 Ltd, (KCU 1990 Ltd) uliofanyika leo tarehe 3/05/2012 katika ukumbi wa hoteli ya Coop iliyoko katika pwani ya ziwa Victoria eneo la Kastamu.
Mkutano huo wa KCU 1990 Ltd ni mkutano wa mwaka wa kufunga msimu wa mwaka 2011/12 na kufungua msimu mpya wa kununua kahawa wa 2012/13. Pia kupisha makisio ya msimu mpya wa kununua kahawa , pia katika mkutano huo unafanyika uchaguzi wa wajumbe wa bodi kwa kutoa theruthi moja ya wajumbe na kuingiza wapya theruthi moja.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe. Masswe pamoja na kusistiza juu ya vyama kutojihusisha katiak kesi kwenye hotuba yake, pia alisistiza KCU 1990 Ltd kuanzisha mradi wa vitalu vya kahawa ili wakulima wapewe miche ya kahawa ya kisasa na kuondokana na mibuni ya zamani ambayo haina tija tena na hamnufaishi mkulima.
Pia Mhe. Ameziagiza Halmashauri za Wilaya kuhakikisha zinaweka mazingira safi kuhakikisha kahawa inayozalishwa inakuwa safi nakukidhi viwango vya soko la kahawa duniani jambo ambalo litamfanya mkulima anufaike na kahawa yake kwa kupata bei inayolingana na thamani ya kahawa yake. Pia aliwakumbusha na kuwasistiza viongozi wa KCU 1990 Ltd kuboresha bei ya kahawa msimu huu wa 2012/13 ili kukomesha tatizo la magendo ya kahawa mkoani Kagera.
Uzinduzi wa Jengo la KCU 1990 LTD
Vilevile Mhe. Massawe hakusita kukwakumbusha wajumbe wa mkutano huo kutowachagua viongozi ambao wanaomba kura kwa kutoa rushwa. Kuweka mchwa kwenye uongozi watataka fedha zao zirudi pale wanapopata madaraka. Ni vyema kujitahadharisha sana na mchwa hao ili kulinda chama. Pia aliwapongeza wajumbe wa bodi kwa kumsimamisha mjumbe mmoja ambaye aligundulika kuwa mbadhilifu wa fedha za chama.
MASUALA MTAMBUKA: Katika mkutano huo Mhe. Massawe alitumia nafasi hiyo kuongelea masuala mtambuka katika mkoa wa Kagera ili mkoa upige hatua ya maendeleo mbele, jambo la kwanza aliwaomba na kuwasistiza sana wananchi wa mkoa wa Kagera kuacha Uvivu.
(Obunafu, Orwango na Kamunobere) Uvivu, Roho mbaya na Hitima ili wawekezaji waweze kuja Kagera na kuwekeza.
Lakini pia wananchi wa Kagera wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha kunywa pombe na kahawa wakati na muda wa kazi, Mhe. Massawe alitolea mfano Nchi ya Korea Kusini kuwa wao wanafanya kazi masaa 18 na wana maendeleo makubwa sana . Pia Mhe Massawe ilitaja adui wa amani na maendeleo kuwa ni pamoja na Ujambazi wa kutumia siraha, Wezi wa mifugo,Unyasasaji wa kijinsia, Mimba za Utotoni, Kujischukulia sheria mikononi, Kuchoma moto.
Usafi wa nyumba katika Manispaa ya Bukoba, Mhe.Masawe amesema kuwa paa za nyumba katika Manispaa ya Bukoba zimechakaa sana na ni pamoja na majengo ambapo nyumba hizo zinahitajika kupakwa rangi mpya pamoja na paa za nyumba aidha kubadilishwa au kupakwa rangi upya.
Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha KCU 1990 Ltd umehudhuriwa na awajumbe wapatao 328 kutoka katika vyama vya msingi vipatavyo 126. Pia mkutano huo umehudhuliwa na wageni waalikwa kutoka katika mkoa na nje ya mkoa wa Kagera. Pamoja na mkutano huo umefanyika uzinduzi kuweka jiwe la msingi katika jengo jipya la oropha tatu linalojengwa na KCU1990 Ltd kwa gharama ya zaidi ya milioni 740 katika mtaa wa Haki barabara ya One way katikati ya mji wa Bukoba.
Na: Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA