Bukobawadau

UZINDUZI WA HUDUMA MPYA YA KUUZA TIKETI ZA MABASI KWA MTANDAO

Bw. Albert Muchuruzi Mkurugenzi wa kampuni ya Mobile Ticketing Limited akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari Maelezo wakati walipotambulisha huduma yao mpya ya kuuza tiketi za mabasi kwa mtandao jijini Dar es salaam, kushoto ni Costa Kamilija ofisa maendeleo ya biashara, na kulia ni Nancy Mtenga mwakilishi wa kampuni ya mabasi ya Metro.
Afisa maendeleo wa biashara  ndg Casta Kamilija  akionyesha bango linalo onyesha jinsi ya kununua tiketi kwa mtandao.

 Kampuni mpya ya Kitanzania ijulikanayo kama Mobile Ticketing Limited kwa ushirikiano na Mitandao ya Simu ya  Vodacom,Airtel, Zantel na Makampuni ya Mabasi inayofuraha kuwatangazia kuwa inazindua huduma mpya na rahisi ya kukata ticket za mabasi yaendayo mikoani na nchi Jirani kupitia simu ya mkononi. Huduma hii inajulikana kwa Jina la "Ticket popote" ni ya kipekee na ya kwanza kuzinduliwa hapa nchini Tanzania.

Mobile Ticketing Limited inatambua usumbufu waupatao abilia  wakati wanakata kusafiri za mabasi ya Kwenda Mkoani na Nchi Jirani . Huduma hii inalenga kuondoa utaribu wa kizamani uliokuwa na usumbufu ambapo abilia alitakiwa kufika kwenye ofisi za basi husika ili kukata ticket, kuzidishiwa nauli na madalali (wapiga debe) hasa wakati wa msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka, kuuziwa ticket moja mtu zaidi ya mmoja au kuuziwa ticket ya basi lisilokuwa na safari. Huduma hii mpya ya kukata ticket kwa njia ya ki”electronic” itasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa huu usumbufu, ambapo abilia ataweza kupata tiketi popote pale alipo, kama atakuwa anapata mtandao wa simu husika..
Next Post Previous Post
Bukobawadau