WAKULIMA WA KILIMO CHA KISASA KUTOKA NCHINI AFRIKA KUSINI WATEMBELEA TANZANIA
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon akizungumza na waandishi wa habari pamoja na kuwakaribisha wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka makampuni 13 ya nchini Afrika Kusini ambao wamekuja Tanzania kwa ajili ya matembezi ya kujifunza mbinu mbali mbali za kilimo na kuangalia fulsa za kuikwamu Tanzania katika mpango wa kilimo kwanza.
Mkutano wa waandishi wa habari pamoja wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka Afrika Kusini.
Mkutano wa waandishi wa habari pamoja wakulima wa kilimo cha kisasa kutoka Afrika Kusini.
Katibu Mtendaji wa Tanzania Youth Agriculture Foundation (TYAF) Bw. Gasper Mahekula akitoa maelezo machache ya taasisi yao mbele ya wakulima kutoka nchini Afrika Kusini pamoja na waandishi wa habari ambapo aliwakaribisha wageni hao kuwekeza katika kilimo. Wa kwanza kulia ni Mtaalam wa Mambo ya Utawala wa Kilimo wa Kampuni ya IIQ ya Afrika Kusini Bw. Ockie Olivier ambaye ameongozana na wenzake wakifuatilia mkutano huo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. Braam Coetnee (kushoto) wakiwa na mmoja ya wenyeji wao (katikati) pamoja na Kiongozi anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. John Luscombe jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Africa Century 4 Development (CC) Fred Simon akifanya mazungumzo na waandishi wa habari mara baada ya mkutano jijini Dar es Salaam. Kiongozi anayehusika na mambo ya nje ya Kampuni ya Konsortium, Afrika Kusini Bw. John Luscombe akifanya mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya mkutano jijini Dar es Salaam. Picha/www.kajunason.blogspot. |