Bukobawadau

WAKUU WAPYA WA WILAYA 6 MKOANI KAGERA WAAPISHWA HII LEO









HABARI KAMILI NA MAELEZO YANAFUATA HIVI PUNDE






Wakuu wa Wilaya wateule wa mkoa wa Kagera wameapishwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe na kuwa Wakuu wa Wilaya saba za mkoa wa Kagera. Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa leo tarehe 18/05/2012 kuanzia saa 4:00 asubuhi mpaka saa 6:30 adhuhuri.

Wakuu wa wilaya walioapishwa leo ni Bibi Zipporah L. Pangani (Bukoba), Bw. Lembris M. Kipuyo (Muleba), Bibi Darry Rwegasira (Karagwe), Lt. Col. Benedict Kitenga (Kyerwa Wilaya Mpya), Constantine J. Kanyasu (Ngara), Richard Mbeho (Biharamulo), na  Kanali Issa E. Njiku (Missenyi).

Katika hotuba yake baada ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya Mkuu wa Mkoa Mhe. Massawe aliwasisitiza sana Wakuu hao kunyesha imani yao kwa Mhe. Rais aliyewateua kwa vitendo akimaanisha kuwatumikia wananchi kwa vitendo kama Rais alivyoonyesha imani kwao kwa kuwateua ili wawatumikie wananchi.
Pia amewakumbusha kufanya kazi kwa kufuata sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ilani ya chama kilichopo madarakani pamoja na nyaraka na maagizo mbalimbali ya Mhe. Rais katika kutekeleza na kusimamia shughuliza za maendeleo katika wilaya zao. Pia kusimamia na kuhakikisha matumizi na mapato ya fedha za halmashauri zinatumika kama ilivyopangwa.

Vilevile Kutunza mazingira, Kupambana na wahamiaji haramu, Kushiriki katika usafi,na kupambana na wala rushwa wa fedha za serikali ni mambo muhimu ambayo Mkuu wa Mkoa amesistiza sana kwa Wakuu wa Wilaya wapya kuyashughulikia katika wilaya zao ili kuhakikisha mkoa wa Kagera unapiga hatua ya maendeleo mbele.
Aidha katika kuwatia hamasa ya kufanya kazi, Mkuu wa Mkoa Mhe. Massawe alitaja baadhi ya vivutio na rasilimali za mkoa wa Kagera. Alisema Kagera kuna hali nzuri hewa, huhitaji kuwa na viyoyozi katika mkoa wa Kagera, pia mvua zinanyesha za kutosha na wastani bila kuleta madhara. Vilevile kuna ardhi nzuri yenye rutuba ya kutosha kuzalisha chakula kwa wananchi wa mkoa wa kagera na mikoa ya jirani.

Mkuu wa mkoa alimalizia hotuba yake kwa kuwakumbusha na kuwahamasisha wananchi wa mkoa wa Kagera kukubali kushiriki kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka huu mwezi Agosti 26, 2012. Pia amewahimiza wananchi kuendelea kufanya usafi katika maeneo yao ili kuuweka mkoa wa Kagera safi.
Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya waloapishwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Issa E. Njiku wamemhaidi Mkuu wa Mkoa kujituma katika kufanya kazi zao na wamehaidi kufanya kazi kama timu moja ili kuhakikisha mkoa wa Kagera unapiga hatua haraka za maendeleo na kuinua zaidi kipato cha mwananchi wa mkoa wa Kagera.

Na Afisa Habari Mkoa Kagera
Mkuu wa Mkoa Mh. Massawe akiteta jambo na Mh. Meya Anathory Aman
Wakuu wa wilaya , viongozi wa Manispaa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa.

NAENDELEA
Next Post Previous Post
Bukobawadau