DK. STEVEN ULIMBOKA AJERUHIWA VIBAYA NA WATU WASIOJULIKANA.
- Rahimu Bora uchungu wanajisikia madktari wenzake ndo sisi tunavyojisikia. ndugu zetu wanakufa
- Elina Lutainulwa its too bad thou kushindana na mtu aliyeshika mpini na wewe umeshika makali ni mbaya sana
- Andrew Peter Kato unauzunguka mbuyu tu Rahimu Bora, why dont you send your meseji straight! Kwani Ulimboka ndiye kawaletea wazazi wako matatizo ya vibofu, stroke na moyo? Hizo lawama itupie serikali yako
- Rahimu Bora what is big pic. @Gordon ,@Andrew kato swala sio kuzunguka watu wanauchungu km uuguliwi shukuru Mungu.
- Andrew Peter Kato I feel very sorry for that level of myopic thinking and attitude my friendZitto KabweNimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.
Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.
Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa ‘agente provocateure‘ kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.
Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.
Nimemuomba Waziri kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’
Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
- Beatrice Msacky Halafu haya Mambo ya nayaonaga kwenye Movie tu. Duh live live . Hata Mungu Hapendi Jamani sio vizuri
- Waziri wa mambo ya ndani Dr. Emmanuel Nchimbi amesema serikali itachunguza na kuwakamata waliohusika na kumteka na kumpiga Dr. UlimbokaRahimu Bora Wazazi wangu walinifundisha ukiwa kwenye mgomo; Usikae mbele wala nyuma ; mpk leo sijui mantiki ya maneno yao
- Osward Modest . . . . . . . is this a solution? suala ambalo mtu hulitenda kama hatua ya mwisho hudhihirisha kwamba uwezo wake wa kufikria umeishia hapo. tunaelekea wapi?
- Alex Lubida Pole sana ndugu Ulimboka, huu ni unyama mbaya sana