MASHINDANO YA UMISSETA MKOA WA KAGERA YAZINDULIWA RASMI KATOKE- MULEBA
Wanafunzi wa sekondari wakiandamana kuelekea kwenye viwanja vya Katoke katika Uzinduzi
Makamu Mwenyekiti wa UMISSETA Mkoa wa Kagera Bw. Renatus Bamporiki Akitoa neno la Utangulizi na Ufafanuzi wa Mashindano hayo kwa Mgeni Rasmi
Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Lembrisi Kipuyo Akisoma Hotuba ya Ufunguzi kwaniaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Makamu Mwenyekiti wa UMISSETA Mkoa wa Kagera Bw. Renatus Bamporiki Akitoa neno la Utangulizi na Ufafanuzi wa Mashindano hayo kwa Mgeni Rasmi
Mkuu wa wilaya ya Muleba Mhe. Lembrisi Kipuyo Akisoma Hotuba ya Ufunguzi kwaniaba ya Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
Ufunguzi wa mashindano ya Umoja wa Michezo na Sanaa Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) mkoani Kagera umefanyika rasmi katika Chuo cha Walimu Katoke Wilayani Muleba leo tarehe 05/06/2012. Uzinduzi huo wa michezo ya Umiseta inajumuisha wanamichezo 640 kutoka katika Wilaya saba za mkoa wa Kagera pia mashindano ya michezo hiyo yanafanyiaka kwa siku nne mfurulizo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Lembris M. Kipuyo aliyesistiza wanamichezo wote kucheza na kushindana bila kuumizana na kucheza kwa upendo na kuzingatia nidhamu kama ambavyo wawapo shuleni kwao.
Mkuu wa mkoa katika hotuba yake alisistiza wanafunzi kuchukulia michezo kama masomo mengineyo na kuzingatia somo hilo kwasababu michezo ni ajira, michezo hutatua migogoro katika jamii mbalimbali, michezo hudumisha utamaduni wa nchi na makabila mbalimbali, aidha michezo huibua vipaji vya watoto.
Pia Mkuu wa Mkoa alisistiza juu ya serikali kuinua maisha ya wananchi wake ifikapo mwaka 2025 (Dira ya maendeleo ya 2025) ambapo alisistiza kuwa michezo ni njia moja ya kuinua maendeleo ya wananchi kwa kupitia ajira. “Michezo ni njia moja wapo ya sehemu inayotegemewa katika kuinua maisha ya mwananchi ifikapo mwaka 2025 kama tutaipa kipaumbele.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa.
Katika mashindano ya UMISSETA mkoa wa Kagera yatahusisha michezo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono, wavu, mpira wa meza, bao, riadha na netiboli michezo hiyo ni kwa wote wasichana na wavulana waliokusanyika kutoka katika Wilaya za Bukoba, Misenyi, Muleba, Ngara, Biharamulo na Chato.
Aidha Mkoa wa Kagera mwaka jana 2011 ulifanikiwa kupata wanafunzi 11 waliofanya vizuri katika ngazi ya Kitaifa na kati ya hoa wasichana wanne waliweza kupata ufadhili wa kwenda kusoma katika shule maalumu za michezo (Sports Academy) Jijini Dar es Salaam, pia mwaka mwaka huu mategemeo ya kuchukuliwa wanafunzi zaidi wenye vipaji ni makubwa kwa jinsi mkoa ulivyojiandaa.