Bukobawadau

MKUTANO WA CHADEMA BUKOBA HII LEO; L wakatare aendeleza M4C-Vua Gamba vaa Gwanda

Mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ukiendelea hii leo
 Anthony Komu Mkurugenzi wa fedha na utawala Chadema Taifa akiwahutubia wadau waliojitokeza kwenye Mkutano wa Chama hicho hii leo. Ndg Komu amesema yeye anatokea Moshi  na wao waliachana na Chama tawala. zamani na mpaka hii leo Moshi wanaongoza kwa kuwa na shule nyingi  hapa nchini, wanaongoza kwa usafi kila mwaka hapa nchini na wana vyuo  vingi na shule kuliko sehemu yoyote nchini na kawahasa watu waachane na Chama tawala
 Lwakatare akiendeleza OPERESHENI Vua gamva vaa gwanda katika viwanja vya Uhuru Mjini hapa ni mkutano ulioweza kutikisa kutoka na Idadi kubwa ya watu walivyojaa.
Ndg Wilfred Lwakatare Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CHADEMA  Taifa akiwahutubia wananchi wa Mjini hapa, kikubwa alichokisema Ndg Wilfred Lwakatare ni juu ya M chakato unao endelea wa Uvunjaji wa soko kuu la Mjini hapa kwa kusema yeye hana ugomvi na Ujenzi wa soko kuu isipokua anahoji juu ya mchakato uliopitishwa pasipo vikao halali vya madiwani wa Manispaa.
Na ameonekana kubeza kauli ya Mh. Nape ya kwamba  ata watu waame vipi bado chama chake kipo vizuri.
Lwakatare amesema hiyo ni kauli ya teja asiyejiweza na kutishia kuua  ile hali hana ubavu ,Ndg Lwakatare kasema Chadema Bukoba wapo katika mchakato wa kujipanga asa katika kata ,mwisho katumia fulsa hii kuendeleza operesheni Vua gwanda vaa gamba na Movement for change kwa kuhuza kadi mpya za chama chake.
 Mdau pichani akipata matukio.
 Anaonekana Mr Bagoka (katikati)akisikiliza yaliyomo ndani ya M4C.
 Wa mwisho nyuma kushoto ni Mama Mwainunu.
Lwaks in action.
Wadau wakifatilia kwa utulivu
 Pichani ni Ndg Silivesta Masinde mwenyekiti CHADEMA Taifa wa baraza la wadhamini wa chama, mkutano huu pia umehudhuliwa na Josephati Isango mwenyekiti Baraza la Vijana Singida pia alikuwepo Kuntu Yusuph Mwenyekiti Baraza la Wanawake mkoa wa Dodoma.
Lwakatare akimkalibisha msemaji wa mwisho Ndg Silvesta Masinde.
Ndg Masinde akiongelea juu ya Mchakato wa Katiba.
Next Post Previous Post
Bukobawadau