Bukobawadau

MSAADA KWA MDAU MWENZETU

habari mdau

awali ya yote napenda kukushukuru na kukupongeza kwa kazi nzuri ambayo umekuwa ukiifanya ya kutuunganisha sie tulio mbali na bukoba unapoweka matukio hapa na sisi tunajisikia kama tupo nyumbani,

baada ya hapo naomba unisaidia kitu kimoja kuna msichana mmoja ni rafiki yangu amekuwa kama mdogo wangu amekuwa akinyanyasika na familia inayomlea wazazi wake wote wlishafariki akabakia analelewa na mama mdogo sasa alipofika high school akamwambia mama yake mdogo naomba nyaraka za wazazi wangu kama death certficate na mengineyo nfatilie mirathi ya wazazi wangu ili pesa hizo zinisaidie mimi na mdogo wangu shule ,basi hilo likwa kosa huyo mama akaanza kumnyanyasa akificha nyaraka zote mpaka vyeti vya huyo mwanafunzi vya form four huyo dada amemaliza form six mwaka jana na akafanaya Application mlimani akachaguliwa lakini ikabidi ahairishe mwaka kwa kuwa hakuwa na vyeti halisi na wala hakupta mkopo kwa kuwa hakuwa na vyeti vya kumuweza kupata mkopo sasa mwaka huu tena mama yake bado hajampa nyaraka zake na hata death certifivcate za wazazi wake ambazo angezitumia kuomba mokopo serikalini na angepata asilimia mia 

mimi binafsi naamini sana katika nguvu ya media, nilikuwa nakuomba yafuatayo

  • nikutumie namba yake kama utaweza ukutane nae na yeye akusimulie upya uso kwa uso ilikama kuna maswali ya kumuuliza umuulize moja kwa moja na uweze kushere nae kati ya njia hizi zipi yuko tayari kuzitumia  
  • kukumkutanisha na mwandishi wa habari yeyote wa tv hapo bukoba ili arushe habari yake huyu mtoto apate msaada wa kisheria
  • au kumpatia contact za mbunge au meya naamnini ni watu wanaoweza kumsaidia kwa haraka 
  • kumkutanisha na shirika la msaada wa sheria ili huyu mtoto apate vyeti vyake 
  • au kuweka ishu zake kwenye blog ili wadau wamsaidie msaada wa sheria kama atakubali 
Next Post Previous Post
Bukobawadau