Bukobawadau

UNITED REPUBLIC OF TANZANIA DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMUNICATIONS


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji 10 wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuanzia jana Alhamisi, Juni 7, 2012.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y Sefue jioni ya leo, Ijumaa, Juni 8, 2012, walioteuliwa ni Ndugu Francis Sales Katabazi Mutungi, Ndugu Sam Mpaya Rumanyika, Ndugu Patricia Saleh Fikrini, Dkt. Gerald Alex Mbonimpa Ndika na Ndugu Salvatory Benedict Bongole.

Wengine walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania ni Ndugu Mathew Pauwa Mhina Mwaimu, Ndugu Jacob C.M. Mwambegele, Ndugu Latifa Mansoor, Ndugu John Samwel Mgetta na Ndugu Joaquine Antoinette De- Mello.

Kabla ya uteuzi wake Ndugu Mtungi alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Ndugu Rumanyika alikuwa Msajili wa Baraza la Rufani la Kodi, Ndugu Fikirini alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Ndugu Ndika alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sheria Tanzania na Ndugu Bongole alikuwa Naibu Msajili Mwandamizi, Mahakama Kuu.

Ndugu Mwaimu alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Haki za Binadamu, Ndugu Mwambegele alikuwa Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Ndugu Mansoor alikuwa Wakili katika Latifa Law Chambers, Ndugu Mgetta alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani na Ndugu De-Mello alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Juni, 2012
Next Post Previous Post
Bukobawadau