KUTOKANA NA TUHUMA ZINAZOMKABILI MH. ZITTO KABWE FUATILIA KAULI ZAKE NA MITAZAMO YA WADAU MBALIMBALI!!!!!
- najua niliumiza watu wengi sana. Wanajitahidi niwe Kama wao credibility wise. Wame team nje ndani ha ha ha .
- yeyote akionesha ushahidi, chembe tu ya ushahidi, kwamba nimekula rushwa, sitasubiri a minute, nitawajibika
- baadhi ya wabunge wanapika tuhuma kwa sababu 1) hasira za kupinga posho 2) Urais 2015. Najua Hilo na Dunia ijue hivyo
- nimesema toka jana, sijatetea mtu Bali taratibu. I am a convinction politician kwa hiyo siangalii upepo unaelekea wapi
- niwajibike? Kwa lipi? Minong'ono ya masuala ya
#tanesco? Mwenye uhakika kuwa kwa namna yeyote nina makosa aseme. ( ZITTO KABWE )
"Hakuna hata mbunge mmoja aliyesimama kusema nani amehongwa nini. Mimi binafsi sijahongwa na mtu yeyote wala mimi sijamtetea mtu isipokuwa natetea taratibu kufuatwa," alisema.
Zitto alibainisha kuwa anaamini tuhuma hizo zimetokana na hasira za yeye kupinga posho za wabunge na sasa wameona hilo ndilo eneo la kumkomoa.
"Kwa kuwa ‘my conscious is clear’, (dhamira yangu safi) sina mashaka, uzushi, uongo na siasa za majitaka hizi zitaumbuliwa na ukweli. Hata hivyo, kwa kuwa tuhuma hizo zinasemwa juu juu tu, tutataka vyombo vya dola vichunguze na ikithibitika hatua zichukuliwe," alisema na kuongeza:
"Kwangu mimi naona hizi ni siasa za urais na hasira za posho. Wenye kutaka urais wa vyama vyote na wapambe wao, wameungana kunichafulia heshima yangu. Wabunge wenye njaa ya posho, wameungana kunikomoa. Ukweli una tabia ya kutopenda kupuuzwa. Mwalimu Nyerere (Julius) alisema katika andiko lake la 'Tujisahihishe'.”
Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini(Chadema) alishauri pia Spika wa Bunge kutumia Kamati ya Maadili kuchunguza tuhuma hizo kwa kuwa hazipaswi kuachwa zikapita hivihivi.
JANUAR MAKAMBA; Nani kakwambia siandamwi? Mimi wauaji wangu wananifukuza kimya kimya. Wa Zitto wanapiga mayowe.
KUTOKA KWENYE POST YA WADAU GROUP;