Bukobawadau

SCHOOL BASH OF TALENTS KAGERA 2012 SEASON 2

Mwendelezo wa tamasha la kusaka vipaji  lijulikanalo kama School Bash of Talent Kagera 2012 likichukua kasi ,hivi ndivyo walivyotokelezea Ma MC's wanaojua kile wanachokifanya kuendana na kasi ya kizazi hiki.
Meza wa ma Judge ikiongozwa na Mwalimu Joyce Radio Presenter,  kushoto ni Dj Sley  muziki kwake ni maisha na kulia ni Msanii msomi Evance hakika kila kitu kipo mahala pake chini ya The Slope Promo & Intertainment waandaji wa mchongo huu.
Ni hatari kwa stege washiriki wakionyesha kuchuana
 "Old is Gold"mambo ya Kitime adhalani na katika hili Bukobawadau blog tunapenda kuwajulisha kwamba bado milango iko wazi kwa yeyete anayependa kudhamini mashindano hayo yenye lengo la kuwainua vijana wa hapa hapa.
 Mwanadada huyu  akijijimwaya mwaya kwa kuimba R&B and Soul huku akipaza sauti  Over Whitney Houston.
Swala zima ni kusebeneka.
Kama ambavyo imeshafahamika mashindano haya yanawahusisha wanafunzi na vijana wa kitaa,pichanI ni Msanii wa kitaa akiwapagawisha mashabiki.
Mchakato huu utaendelea Jumapili tarehe 15/7/2018 katika ukumbi wa Coffee Tree Inn Hotel na habari matukio mtaendelea kuyapata humu katika Mtandao wetu!!

KUPATA MATUKIO YA MUDA MCHACHE ULIOPITA GONGA NENO OLDER POST NA KUTUSHIRIKISHA KATIKA MATUKIO WAWEZA KUWASILIANA NASI KUPITIA 0715 505043,0784 50505 NA 0768 397241  Email  bukobawadau@gmail.com na BBM PIN  2794A145.


Next Post Previous Post
Bukobawadau