KANDA YA ZIWA MAGHARIBI YAIBUKA BINGWA WA SOKA UMITASHUMTA
Timu Bingwa Mpira wa Miguu Wanaume Kanda ya Ziwa Magharibi (Kagera na Kigoma) Wakishangilia Ushindi Baada ya Kupata Kikombe cha Ubingwa Kitaifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI Bi Hawa Ghasia Akimkabidhi Kikombe cha Mshindi wa Kwanza Kitaifa (Bingwa) Hernest Musa Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu Kanda ya Ziwa MAgharibi ( .Kigoma na Kagera ) Katika Mashindano ya UMITASHUMTA 2012 Kibaha Mkoani Pwani.
Afisa Michezo Mkoa wa Kagera Bw. Kepha Elias Aliyesimama wa Kwanza Kushoto Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Timu ya Wasichana Mpira wa Miguu Kibaha Mkoani Pwani.

Timu ya mpira wa miguu ya wanaume ya walemavu (Viziwi) Kanda ya Ziwa Magharibi (Kagera na Kigoma) imeibuka bingwa baada ya kuwa mshindi wa kwanza kitaifa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Ngazi ya Taifa yaliyofanyika Uwanja wa Shirika la Elimu Kibaha mkoani Pwani kuanzia tarehe 1-11/07/2012.
Pamoja na ushindi huo Kanda ya Ziwa Magharibi ilijinyakulia Medali 17 za mchezo wa riadha, Medali 2 za Taaluma, na Kikombe kimoja cha mpira wa wavu baada ya kuwa mshindi wa 3 pamoja na Zawadi ya seti ya jezi. Aidha Kanda ya Ziwa Magharibi imejipatia mchezaji bora kitaifa ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya msingi Mugeza Viziwi kutoka Mkoa wa Kagera Ernest Musa aliyejipatia zawadi ya Mpira.
Wakati huo huo katika Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) yaliyofanyika Juni 18 – 29, 2012 katika kituo hicho hicho Kibaha Pwani, Kanda ya Ziwa Magharibi ilijipatia Medali 2, Medali ya Dhahabu riadha mita 400, na Medali ya Shaba kurusha tufe, pamoja na Vikombe 2 vya nidhamu na usafi.
Aidha Kanda ya Ziwa Magharibi katika michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kitaifa ilishiriki michezo ya riadha, mpira wa mikono, Mpira wa Miguu, Mpira wa Kikapu na Wavu kwa wasichana na wavulana. Michezo mingine ni soka maalum kwa wavulana na netiboli kwa wasichana, vilevile wanafunzi wa shule za msingi walishindana kitaaluma kwa kuzingatia usafi na nidhamu katika michezo.
Kutokana na Mashindano hayo Mkoa wa Kagera uliweza kuibua na kuonesha vipaji vya wanafunzi wake kimichezo na kitaaluma kwasababu asilimia 75 ya washiriki walitoka mkoani hapa. Aidha mkoa umeimarika na kupata wachezaji wengi wanaofadhiliwa kimasomo na wadau wa kuinua maendeleo ya michezo nchini.
Mashindano ya UMISSETA na UMITASHUMTA kitaifa yalishirikisha kanda zipatazo 9 ambazo ni; Kanda ya Dar es Salaam (Kanda Maalum), Kanda ya Mashariki (Morogoro na Pwani), Kanda ya Kaskazini Magharibi (Manyara/Arusha), Kaskazini Mashariki (Tanga na Kilimanjaro), Kanda ya Magharibi (Shinyanga na Tabora), Nyanda za juu (Mbeya na Rukwa), Nyanda za juu Kaskazini (Ruvuma na Iringa), Kanda ya Kusini (Lindi na Mtwara), na Kanda ya ziwa (Mwanza na Mara).