NANE NANE 2012 MKOA WA KAGERA KUADHIMISHWA KYAKAILABWA.
Picha za Wanyama na Kilimo Mambo Muhimu Ambayo Hayakosi Katika Uwanja wa Kyakailabwa Katika Maonyesho ya Nane Nane
Wananchi wa Mkoa wa Kagera mnaombwa kushiriki katika maadhimisho ya maonyesho ya NANE NANE mwaka 2012 Katika uwanja wa Kyakailabwa nje kidogo ya mji wa Manisaa ya Bukoba.
Maonyesho hayo yameanza leo tarehe 01/08/2012 na yataendelea mpaka kilele ambacho ni tarehe 08/08/2012. Uzinduzi rasmi utafanyika tarehe 03/08/2012 siku ya Ijumaa kuanzia asubuhi saa 3:00
Katika maonyesho hayo yanayoshirikisha wadau mbalimbali kutoka katika mkoa mzima wa Kagera huonyesha shughuli mbalimbali za kilimo, biashara, ujasiliamali pamoja na burudani mbalimbali.
Wananchi mnakumbushwa kwenda kujionea mambo mbalimbali katika uwanjwa huo wa Kyakailabwa pamoja na kuwapeleka watoto kujionea wanyama mbalimbali, pia na kujiapatia huduma za kununua bidhaa mbalimbali kwa bei nafuu sana na kujifunza shughuli mbalimbali za ujasiliamali na kilimo, tafadhali usipoteze nafasi hii katika msimu wa Nane Nane 2012.
Imetolewa na: Sylvester Raphael,
Afisa Habari Mkoa,
Kagera.