Bukobawadau

SKYLIGHT BAND KUTAWAMBULISHA WAKALI WAO SIKU YA EID MOSI NA PILI NDANI YA GIRAFFE OCEAN VIEW, DAR

-----


 Vijana wa kazi walionyesha staili yao mpya ya kuheza.
NA MWANDISHI WETU 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi na Zena Mohamed ‘Shilole’ wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa bendi ya Skylight wakati wa Sikukuu ya Iddi Mosi. 
 Akizungumza na vyombo vya habari jana kiongozi wa Skylight Band Aneth Kusila ‘AK47’ alisema uzinduzi huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, uliyopo Mbezi Beach. 

AK47 alisema uzinduzi huo utakuwa wa namna yake kutokana na uwezo mkubwa walionao wasanii wanaounda Skylight.

“Mashabiki wote wa muziki Tanzania waje washuhudie vipaji hivyo na jinsi tulivyojiandaa kuwapa burudani ya aina yake,” alisema AK47. 

Skylight Band inaundwa na wakali kama AK47 na Mary Lucos, ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Bongo Star Search (BSS). 

Wengine ni Joniko Flower na Sam Machozi, ambao wote wametoka Machozi Band, inayomilikiwa na Lady Jay Dee. 

Baada ya uzinduzi huo Skylight Band watafanya onyesho jingine kwenye ukumbi huo wa Giraffe siku ya Iddi Pili, ambapo Dj Nelly ataonyesha uwezo kwa kupagawisha mashabiki kwenye maonyesho yote mawili.
Next Post Previous Post
Bukobawadau