WAZIRI SITTA AENDELEA NA ZIARA YAKE WILAYANI KYERWA - MURONGO
Mhe. Sitta Akiwa Ameketi Kwenye KIgoda Tayari Kusimikwa na Wazee wa Karagwe na Kyerwa Kuwa Mzee wa Karagwe.
aratibu za Kusimika zikendelea
iraha za Kitamaaduni za Kinyambo Alikabidhiwa Mhe. Sitta
Mhe. Sitta Akiwa Ameketi Kwenye KIgoda Tayari Kusimikwa na Wazee wa Karagwe na Kyerwa Kuwa Mzee wa Karagwe.
aratibu za Kusimika zikendelea
iraha za Kitamaaduni za Kinyambo Alikabidhiwa Mhe. Sitta
Mhe. Sitta Akiwa Ameketi Kwenye KIgoda Tayari Kusimikwa na Wazee wa Karagwe na Kyerwa Kuwa Mzee wa Karagwe.
Mheshimiwa Samwel Sitta Waziri wa Shirikisho la Afrika Mashariki katika ziara yake mkoani Kagera anaendelea kutembelea maeneo mbalimbali katika Wilaya za Karagwe na Kyerwa na kukutana na makundi mbalimbali ya wananchi pia na kutembelea miradi inayotekelezwa chini ya Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Jana tarehe 28/08/2012 Mhe. Sitta alitembelea kikundi cha Wanawake wajane Wazee na Watoto yatima Wilayani Karagwe ambapo kikundi hicho kilijumuisha Wazee wa Karagwe na Kyerwa waloimsimika Mheshimiwa Sitta kuwa Mzee wa Karagwe.
Baada ya kusimikwa kuwa Mzee wa Karagwe Mheshimiwa Sitta aliwahutubia wanawake wajane, Wazee, watoto yatima na wananchi waliofika kumskiliza. Katika hotuba yake aliwaomba wananchi kuwa makini na viongozi wanaotafuta uongozi kwa kutumia fedha. Pia alikemea tabia ya Viongozi kujilundikia mali na kuwaomba watanzania kurudia maadili aliyoyaacha baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Katika siku yake ya tatu Wilayani Kyerwa Mhe. Sitta ameweza kutembelea mpakani mwa Tanzania na Uganda Murongo na Kikagati Wilaya Isingiro nchini Uganda kujionea mradi wa pamoja wa umeme wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kati ya Tanzania na Uganda ambao utanufaisha vijiji vyote vya pande zote mbili mara baada kukamilika.
Mradi huo wa umeme wa maji ambao utafanyika katika mto Kagera tayari umewekewa msukumo na serikali zote mbili za Uganda na Tanzania ili uweze kuanza kuzalisha umeme baada ya miezi mitatu ijayo. Mhe. Sitta katika ziara yake hiyo alikutana Waziri wa nishati wa Uganda ambaye aliwaakilisha nchi yake pia na mshauri muendelezi wa mradi huo.
Mhe. Sitta alihaidi katika kikao hicho kutia msukumo zaidi katika serikali ya Tanzania ili mradi huo uweze kukamilishwa haraka iwezekanavyo ili wananchi wa pande zote mbili waanze kunufaika . Mheshimiwa Sitta ataendelea na ziara yake Mkoani Kagera kwa Kutembelea mpaka wa Kabanga Wialayani Ngara.
Imetolewa na:
Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa,
Kagera @2012