Bukobawadau

ZAIDI YA SHILLINGI MILIONI 500 ZAPATIKANA KATIKA HARAMBEE YA M4C JIJINI DAR

Chadema jana siku ya Ijumaa walifanya Harambee ya Movement for Change hafla ambayo imefanyika katika Hotel ya Serena Dar es Salaam. Katika Hafla hiyo jumla ya shiling milioni 500 zilipatikana ikiwa shilingi milioni 270 fedha taslimu na shilingi milioni 253 ahadi. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chadema na Wageni mbalimbali waalikwa. Baadhi ya Viongozi waliokuwepo katika hafla hiyo ni Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mh Freemani Mbowe, aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini Mh Godbless Lema, Mbunge wa Arumeru Mashariki Mh Joshua Nassari, Mwenyekiti wa Harakati za M4C Mh Alex Mayunga, Katibu wa Chadema Tawi la Washington DC Mh Isdori Lyamuya na Viongozi wengine mbalimbali.
Next Post Previous Post
Bukobawadau