Bukobawadau

ASUBUHI YA LEO NDANI YA SOKO KUU MJINI HAPA INAONYESHA NDIZI SI HABA!!

Camera yetu ndani ya soko kuu mjini hapa imeshuhudia harakati za wadau wakishusha kwa wingi mikungu ya ndizi kutoka katika maroli aina ya fuso.Ndizi nyingi zinatoka Wilaya ya karagwe.Wilaya inayozalisha kwa wingi mazao ya biashara yanayotosha kuilisha nchi hii na nchi  jirani
Kama inavyo onekana pichani  ni mikungu ya ndizi inayouzwa kwa wastani wa sh 5000 mpaka 10000/=kulingana na ukubwa wa ndizi.
Wadau wakiendeleza libeneke la kushusha ndizi ,kinyumbani wanasema "full kuchwazika"!!
 'Full kuchwazika'inahusika.
Wanaonekana wafanyabiashara wa ndizi wakiendelea kufanya biashara kando kando ya barabarani nje ya soko kuu kitendo kilichozuia magari kupata sehemu ya kuegeshwa  asubuhi hii
Gari lingine likiwa bado limeegeshwa kando kando ya barabara likisubiria kushusha mzigo wa ndizi.
Hivi ndivyo lilivyo soko la ndizi hii leo mjini hapa na hii ni ndiyo ya raha ya mji wetu!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau