Bukobawadau

JAJI MKUU OTHMAN CHANDE AAHIRISHA KESI YA RUFAA YA GODBLESS LEMA

Wananchi wa Arusha mjini wakimsikiliza Kamanda Lema kabla ya kwenda mahakamani leo
 Kamanda Lema wakati anaingia Mahakamani leo.

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi  wao ambaye maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.

Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Next Post Previous Post
Bukobawadau