Bukobawadau

KAMPUNI YA ZACHWA INVESTMENT YAENDELEA NA MCHAKATO WA KUSAKA VIPAJA KWA WASANII WA NYUMBANI

Wakati makampuni mbalimbali nchini yanaendelea na mchakato wa kusaka vipaji vya kuimba, hapa Mjini Bukoba Kampuni ya Zachwa Investment inaendelea na mchakato wa kusaka vipaji kwa ajili ya kucheza filamu,Mchakato huo umeendelea kwa siku ya jana katika ukumbi wa Linas Night Club.

Meza ya majaji katika usahili huu kutoka kushoto ni Jaji mkuu Bi Regna Zachwa, Bi Abera Kamala ambaye ni mkufunzi katika tasnia hii na wa mwisho ni Bi Jane Zachwa.
Kushoto ni Mgeni Rasmi Ndg Philbart Nyerere na kulia ni Mkurugenzi wa Zachwa Investment Ndg Mganyizi.

Washiriki wakiingia ukumbini kwa burudani ya nyimbo kutoka kwa mmoja wa washiriki pichani kulia.
Hakika wadau wengi wenye vipaji vya kuigiza wameweza kujitokeza ,pichana wanaonekana wakiendelea ku bumpha kufurahi na kucheza  kabla ya kufanya utambulisho mmoja baada ya mwingine.
Msanii mmoja baada ya mwingine katika utambulisho na tunatamani tuweke picha zao wote mmoja mmoja ili mdau uweze kuona asa kwa wale wanaopenda wingi wa picha ila ukurasa wetu unabanwa na taratibu.
Baadhi  ya mashabiki na kadli muda unavyokwenda ndivyo ukumbi unavyozidi kujaa,na bukobawadau tupo eneo husika  kuakikisha tunatoa ushirikiano kwa wasanii wa ndani na kukufikishia wewe mdau msomaji kile kinacho jili mwanzo hadi mwisho
Mzee Msafiri naye ameweza kuhudhulia mchakato huu.
Meza kuu ya majaji wakiendelea na usahili na kuakikisha wanatenda haki katika utoaji wa maksi kwa washiriki husika.
Mashabiki wakifuatilia kwa umakini burudani zinazoendelea kutoka kwa wasanii.
 Ni kundi zima la Moses Mnyama likiendelea kutoa Burudani
Next Post Previous Post
Bukobawadau