Bukobawadau

MARUK VANILLA FARMING AND PROCESSING (MVFP) LTD




Kwa mara nyingine tena, msimu huu Maruk Vanilla Farming and Processing (MVFP) Ltd wamedhihirisha kuishinda ahadi yao kwa kufanya manunuzi ya vanilla mbichi kwa malipo ya papo hapo kwa pesa taslimu.
Malipo-Pesa
MVFP Ltd ilianzishwa kama kikundi cha wakulima chenye malengo ya kuanzisha, kukuza na kuvumisha mazao mbadala ya Biashara mkoani Kagera. imepitia michakato ya urasimishaji toka kikundi kwenda jina la Biashara na mwaka 2008, MVFP ilisajiriwa na rajisi wa Makampuni na Biashara kama Kampuni yenye hisa zenye ukomo wa madeni.

Toka kuanzishwa, Kampuni imeweza kutoa mafunzo bora ya ukulima na usindikaji wa zao la vanilla kwa ngazi ya awali kwa wakulima zaidi ya 500. 
Wakulima baada ya Mafunzo
Wananchi katika kijiji cha Bulinda-Maruku, Kanyangereko wanafaidika na uwepo wa makao makuu ya kampuni hii kijijini mwao. Wanakijiji wapatao watano (5) wamepata ajira za kudumu
Ajira kijijini Bulinda
Na wengine zaidi ya 15-25 hupata ajira za muda katika msimu wa mavuno. Ajira hizi ni mbali na nafasi za uwakala wa manunuzi zisizopungua 20 ambazo hutolewa kwa wakazi wenyeji katika maeneo ambako MVFP Ltd hununua vanilla. 
Mawakala wa ununuzi wakiwa kazini
Hivi karibuni MVFP Ltd imekamilisha makubaliano yaliyoiwezesha kufungua kituo cha manunuzi na ukaushaji wa vanilla mjini moshi. Pia imeingia makubalinao ya kuiuzia kampuni toka Hispani vanilla yote inayoweza kuzalishwa na kukusanywa na MVFP Ltd Tanzania. Bado kuna changamoto ya uzalishaji mdogo usiofikia mahitaji katika masoko ya kimataifa.
Mazungumzo na makubaliano-Moshi
MVFP Ltd imeweza kupata masoko ya uhakika baada ya juhudi kubwa ya uongozi chini ya Mwenyekiti Murshid Hassan Byeyombo kuwekeza katika ziara za maonyesho ndani na nje ya nchi na pia kufanya matangazo katika mitandao mbalimbali ya Kimataifa ya viungo vya chakula.
Ziarani German
Mfumo wa Biashara wa  MVFP Ltd umekuwa ukiwavutia wadau mbalimbali wa maendeleo. Hii imewapa fursa ya kufanya kazi na Tasisi mbalimbali za serikali na mashirika ya maendeleo. Na hivi karibuni MVFP Ltd itaanza kufanya kazi na Belgium Technical Cooperation (BTC) katika kuinua zao la vanilla. 
Mazungumzo na BTC
Mazungumzo na ARI
Kusonga kwa jitihada za MVFP Ltd kwa mafanikio kunachangiwa na MVFP kuwa chombo kilichoanzishwa na wakulima wenyewe kusimamia maslahi ya mazao wanayozalisha wenyewe. Kila mara wadau wa MVFP hukutana kujadili mambo mbali mbali ya kuinua mazao wanayobuni na kuzalisha. 
baada ya Mkutano wa Wadau
MVFP Ltd iko katika hatua za mwisho kuanza usindikazi wa viungo mbalimbali. Ifikapo mwezi wa kumi mwaka huu MVFP itakuwa imeingiza sokoni bidhaa za viungo kama Masala za aina tatu zinazochanganya kiungo cha vanilla.

Uongozi wa MVFP Ltd unawasisitiza wakulima kutong’oa miche ya vanilla na badala yake waongeze nguvu katika kupanda mishe mipya maana mambo yanaendelea kuwa mazuri kwa bei kuimarika na kumjali mkulima. Na pia wakulima wanashauriwa kutolaghaika kuuza mazao yao kwa mkopo maana thamani ya kiwango cha pesa kinachopaswa kulipwa leo si sawa na thamani ya kiwango kile kile kikilipwa kesho kutwa. 
UONGOZI WA MVFP LTD

MWISHO  NDG MDAU  TUNAZIDI KUKUOMBA  UTUPE USHIRIKIANO KWA KUTUTUMIA HABARI AU MATUKIO YENYE TIJA KUTOKA POPOTE PALE ULIPO PIA KUMBUKA KUTUSUPORT JAPO KWA KUWA FOLLOWERS , JIUNGE NASI KUPITIA SEHEMU HUSIKA KWA KUTUMIA EMAIL YAKO KWANI TUKIPATA IDADI INAYOYORIDHISHA YA MEMBER NI CREDIT KWETU KIUTENDAJI NA KATIKA HILI TUNAOMBA TUFANYE KUAMASISHANA ILI TUWEZE KUFIKIA MALENGO YETU TUNAAMINI CHANGAMOTO BADO NI KUBWA SANA !!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau