Bukobawadau

NI SAWA NA THRILLER KWA MADRID BAADA YA BAO LA CRISTIANO RONALDO KUPELEKEA USHINDI WA 3-2 DHIDI YA MAN CITY

Mchezaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akionyesha umakini katika maamuzi ya mwisho.
Klabu ya Soka ya Manchester City, imeianza vibaya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya, baada ya kukubali kuachia uongozi wa mechi mara mbili na kujikuta wakiangukia pua kwa kulala 3-2 dhidi ya miamba wa Uhispania Real Madrid.
City, ambao kipindi cha kwanza walitumia muda wao mwingi kujihami na hivyo kulifanya pambano hilo kuwa la upande mmoja zaidi, walifunguka kipindi cha pili na kuufanya mchezo huo kuwa wa kuvutia zaidi, ambapo mara mbili waliweza kuongoza mechi, lakini kutokuwa kwao makini kukasababisha mara zote hizo kurejea kwa mabao hayo kabla ya kukubali kulala kwa bao la Cristiano Ronaldo KUTUPIA bao la tatu katika dakika  ya mwisho kabisa.Ujio wa bao hilo naufananisha na thriller ya Michael Jackson.

Next Post Previous Post
Bukobawadau