Bukobawadau

NYOTA YA MDAU CAPTAIN KHALID YANG'AA KATIKA TASNIA YA UIGIZAJI COMEDY!!!

Katika hali ya kushangaza Mdau Khalid Hussen Kaitaba pichani kushoto ambaye mwanzo alijulikana kama kama rapper mkali ndani ya manispaa ya Mji Bukoba na badae kujikita katika kazi ya uandaji muziki (producer) akitumia jina la Kdee,ila kwa sasa ameacha  na kujikita zaidi katika masomo na sasa anachukua degree ya marketing nchini  Singapore.
Mdau Captain Khalid pichani kushoto  katika jitihada zake kusaka pesa,chapaa au mkwanja  kama ilivyo kawada ya utafutaji ameamua kutumia nafasi anayo ipata baada ya masomo yake  kujikita moja kwa moja  katika  mchezo wa Comedy badala ya sanaa ya muziki kama ilivyokua hapo siku za nyuma ,Pichni anaonekana na wenzake wakali wa  kuchekesha kupitia 'stand up comedy'
 Katika maongezi na Bukobawadau Blog, Captain Khalid amejaribu kutoa ufafanuzi kuwa Stand up Comedy ni  aina ya uchekeshaji ambayo msanii ufanya kuongea na watu/mashabiki ucheka na kufurahia,anasema  ni soko kubwa na gumu ila ikikubali mtu unapata pesa na mafanikio makubwa sana,mfano wapo akina Rassel Peters, Kevin Hart, Chris Tucker, Chris Rock, Eddy Murphy na wengine wengi katika tasnia hii ya filamu.
Captain anaendelea kwa kusema kuwa  alianza kupenda fani hii na kupata mafunzo na taratibu alifanya maonyesho katka chuo chake kwa kufanya katika chuo chake na badae akawa anafanya katika mighahawa na bars na mara kwa mara katika comedy clubs.Mpaka hivi tayari kesha pata shavu naameanza kufanya matamasha katika  "theatres"na anapata miariko ya hapa na pale kama Malaysia,Singapore,phillines na HongKong.
Kuonyesha umahiri wake mwanzoni kabisa alipokea tuzo ya ''best upcoming comedian'' msanii bora chipukizi wa vichekesho.Tuzo anayokabidhiwa na Pro.Dr.Jamaludin ambaye ni mkuu wa vyuo nchini Singapore
Staili mpya ya uvaaji wa msanii Captain Khalid
Kikubwa juu ya yote Captain Khalid mtoto wa Mdau Hussein Kaitaba mchezaji wa mpira wa miguu zamani RTC Kagera, Balimi , FC,na Rweru Eagles anapenda kutumia jamvi hili la kinyumbani zaidi  kumshkuru   Mwenyezi Mungu kwa kila kitu, na kusema yeye  si chochote bila mama yake Mzazi!!!
Captain Khalid akiwajibika jukwaani na kwa waleo watakao penda kujua maendeleo yake na baadhi ya show zake mnaweza kutembelea page yake.www.facebook.com/CaptainKhalidComedy

BUKOBAWADAU BLOG TUNAMPONGEZA CAPTAIN KHALID NA TUNAJIVUNIA MAFANIKIO YAKE!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau