SHEREHE ZA KULITABARUKU KANISA KATOLIKI JIMBO LA BUKOBA MJINI BAADA YA UKARABATI MKUBWA ULIOCHUKUA MIAKA 17 KUFANYIKA 7/10/2012 NA MAZISHI YA MAREHEMU MWADHAMA KARDINAL RUGAMBWA NI 6/10/2012
Shughuli ya kuzika masalia ya mwili wa Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa ambaye alikuwa Kardinali wa kwanza mwafrika itafanyika rasmi katika Kanisa la Jimbo Katoliki la Bukoba tarehe 6/10/2012 ikiwa ni miaka 15 tangu alipozikwa kwa muda katika kanisa la Kashozi.
Tarehe 7/10 /2012 kutafanyika sherehe za kulitabaruku Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Mjini baada ya ukarabati mkubwa uliochukua miaka 17.Shughuli ya kuzikwa upya kwa masalia ya Marehemu Kardinali Rugambwa itakwenda sambamba na sherehe za kuadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwake.
Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa,aliyekuwa Kardinali wa kwanza Mtanzania na Mwafrika alifariki dunia 8/12/1997 na kuzikwa tarehe 17/12/1997 kwa muda katika Kanisa Katoliki lililopo Kashozi Wilaya ya Bukoba Vijijini kutokana na ukarabati uliokuwepo katika kanisa hili pichani na sasa unakamili ni Kanisa la Jimbo Katoliki Bukoba.
Marehemu Mwadhama Kardinali Laurean Rugambwa alizaliwa tarehe 12/7/1912 katika eneola Rutabo Kamachumu Wilaya ya Mulebwa na alikuwa Padri 12/12/1947 na aliteuliwa kuwa Kardinali 23/3/1960.

Shughuli hizi zinatarajiwa kuhudhuriwa na watu zaidi ya 10,000 kutoka nje ya Bukoba,viongozi mbalimbali pamoja na maaskofu kutoka Ulaya,Kenya,Uganda, Burundi, na mabalozi mbalimbali na viongozi wakuu wa nchi ni sehemu ya Waalikwa!!.