HAPA NA PALE NA CAMERA YETU MSIBANI MWANZA NYUMBANI KWA MAREHEMU (SACP) LIBERATUS BURLOW
Watu wanajongea polepole nyumbani kwa Marehemu Liberatu Burlow huku wakiwa hawaamini kilichotokea.
Nyumbani kwa Marehemu Liberatus Burlow aliyekuwa Kamanda wa Police Mkoa wa Mwanza
aliyeuwawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi.
Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili.
Ni huzuni tupu,bado ni mapema sana kamati zinaundwa na mikakati inapangwa juu ya kukabiriana na Msiba huu Mkubwa.
Marehemu Liberatus Barlow
Bukobawadau blog tutaendelea kukujulisha kinachoendelea kuhusiana na Msiba huu Mkubwa wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP), Liberatus Barlow.