KATIKA UTAFUTAJI WA MAARIFA MDAU ALEX ASIEL APATA NAFASI YA KUFIKA NCHNIINDIA
Katika moja ya mikutano mdau Alex akijaribu kuelezea mada mbalimbali.
Pichani anaonekana Mdau Alex akijaribu kuelezea mambo mbalimbali kuhusu Tanzania. Pia anapata kuelezea maana halisi ya rangi za bendera ya Taifa.
Katika pitapita zake anashuhudia mafunzi haya karate,ambayo ndio mwanzo wa akna Anil Kapoor au Raju kumar kwa sasa Mithun Chakraborty kwa kizazi chetu.
Mambo yetu yale kudance.
Mdau alipata wageni nyumbani, vijana wahindi walio katika industry ya IT, hakika anakiri alijifunza mengi toka kwao.
Baada ya kazi mdau Alex anapata nafasi ya kukutana na vijana wenzake toka nchi za brazil,columbia,australia,england,USA,portugal,korea,greece na kenya ili kubadilishana mawazo.
Mdau akiteta jambo na Camilo.
Kwa jina ni Ganesha. Moja ya miungu inayoabudiwa na waumini wa dini ya Hindu.
Wakati kibongo bongo siku ya mwenge kufika mahali,au ujio wa mheshimiwa flani ndipo upata mapambo ya hivi uko vijjini kwetu , Nchini India hii ni moja ya sikukuu ya dini ya Hindu migomba michanga hukatwa na kutundikwa kwenye mageti, magari, pikipiki na maofisini pia.
Katika sikukuu hizi kila kitu hupakwa rangi na kuwekewa maua kama unavoona.
Mwisho Mdau anasema anamshkuru Mwenyezi Mungu kwa experience aliyoweza kupata mpaka hvi sasa,
Na yote juu ya yote anatumia fulsa hii kuwashukuru wazazi Wake
MR&MRS Asiel Evarist ,hapa nyumban anajulikana kama Mzee Siel (mfugaji)kwa upendo wao na support walioweza kumpa.
Hakika nafasi hii imembadili sana kimawazo yeye kama kijana kwa sababu anapata
kujifunza mambo mengi toka kwa watu mbalimbali.
ASANTENI NDILO NENO SAHIHI LILILOTUMIKA!!