Bukobawadau

MVUA KUBWA ILIYOAMBATANA NA UPEPE YAEZUA NYUMBA

Mvua kubwa iliyonyesha hii leo mjini hapa  ikiambatana na upepo mkali kama kimbunga  sambamba na Radi za hapa na pale imesababisha uharibifu mkubwa wa mali za watu majumbani hasa vifaa vya umeme na kusababisha jamii kupata hasara pia imeangusha miti, migomba na kuezua majumba.
 Maafa haya yametokea kijiji Cha Buhembe, pichani ni banda la kuonyeshea video Mali ya Mdau Mzee Katemana likiwa limekumbwa na Upepo.
Madhara mengine yametokea maeneo ya Kahororo, Kibeta na Ijuganyundo.
Nyumba mojawapo ambayo paa lake limeezuliwa na upepo maeneo ya Buhembe umbali wa km 5 kutoka Mjini Bukoba.

BADO ATUJAWEZA KUPATA TATHIMINI KAMILI JUU YA HASARA ILIYOTOKANA NA MVUA HII
Next Post Previous Post
Bukobawadau