MWASHAMU BABA ASKOFU NESTORY TIMANYWA ABARIKI UZINDUZI RASMI WA WAZO LA MRADI MKUBWA WENYE LENGO LA KUMUENZI MAREHEMU KARDINALI RUGAMBWA.
Ni majira ya saa 7 mchana wa leo tarehe 16/10/2012.Ikiwa ni muda mchache baada ya misa maalumu ya familia ya Mzee James Rugemalira ya kumuombea marehemu Mama yao Ma Auleria Koburungo Muganda na kufuatia shughuli ya kihistoria katika kanisa la Bunena ni uzinduzi rasmi wa wazo la mradi wenye lengo la kumuenzi Marehemu Kardinali Rugambwa.
Mwashamu Baba Askofu Nestory Timanywa, Askofu Mkuu wa Jimbo la Bukoba akikata utepe,katika shughuli ya kubariki uzinduzi wa wazo la mradi unaopendekezwa kuitwa LAURIAN CARDINAL RUGAMBWA MEMORIAL BUNENA LAKE VICTORIA ROCK BEACH PILGRIMAGE RESORT PROJECT.
Anaonekana mmoja wa watoa wazo pichani Mdau James Buchard Rugemalira akiongozana na Mwashamu Baba Askofu Nestory Timanywa
Mh.Bernadetha MshashuMbunge viti maalumu naye pia ameshiriki katika tukio hili ,pichani (kushoto) ni Mdau Opaty Henry sehemu ya waalikwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera ni mualikwa katika shughuli hii, pichani anasalimiana na Mwashamu Baba Askofu Method Kilaini-Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba.
Meza kuu kutoka kushoto Mwashamu Baba Askofu Kilaini, Mzee James Rugemalira,Mwashamu Baba Askofu Nestory Timanywa na wamwisho ni Mama Rugemalira.
Sehemu ya wageni waalikwa na Mapadre.
Yupo pia askofu mstaafu Samson Mushema wa Lutheran wa mwisho kulia.
Mc Mwalimu Lubozi akisogeza kipaza sauti kwa Mwashamu Baba Askofu Timanywa.
Akiongea kwa hisia Mwashamu Baba Askofu Nestory Timanywa ameanza kwa historia ya makasa ,Baba askofu Timanywa amesema tangu mwaka 1910 Bunena limekua kanisa kuu la Jimbo.pia amegusia makanisa ya kashozi, Rubya, Mugana, Kagondo na Katoke.
Waumini wakimsikiliza Baba Askofu Nestory Timanywa, Askofu Mkuu wa Jimbo la Bukoba.
Sehemu ya wanakwaya.
Muonekano wa nje wadau wakimsikiliza Mwashamu Baba Askofu Nestory Timanywa akibariki uzinduzi wa wazo la mradi wa kumbukumbu ya nwadhama Laurian Kardinali Rugambwa.
Mdau Devis naye ameshiriki.
Mama Benedetha Mshashu akitoa wazo juu ya uwekezaji mjini hapa.
Ukoo wa Bakoba chumbuko la Mzee James Rugemaliraumeshiriki kikamilifu kuanzia wajukuu,vitukuu na vilembwe
Mzee Rweyemamu akisikiliza kwa umakini pembeni yake ni Mdau Jerome.
Washirika wakubwa katika wazo hili lilitolewa na watu mbalimbali wakiwemo na Mapadre.
Kutoka kushoto ni Mr Kamala, Mzee Pius Ngeze na Mdau Ngaiza.
SEHEMU HUSIKA YA MRADI ULIOBARIKIWA HII LEO WA KUMBUKUMBU YA MWADHAMA LAURIAN KARDINALI RUGAMBWA BUNENA LAKE VICTORIA ROCK BEACH PILGRIMAGE RESORT PROJECT.