Bukobawadau

TIMU YA YANGA YAPOKEA KICHAPO CHA BAO 1-0 KUTOKA KWA KAGERA SUGAR

 Ligi kuu ya Tanzania Bara imeendelea hii leo katika uwanja wa kaitaba Mjini Bukoba ambapo timu ya Yanga imeambulia kichapo cha bao 1-0 Kutoka kwa wakata miwa wa Kagera Sugar.
 Mfungaji wa bao la  Kagera Sugar Temmy Alphonce pichani kulia.
Bao la Kagera Sugar limepatikana dk ya 40 kipindi cha pili cha mchezo, Bao hilo limefungwa na mchezaji mahiri mzaliwa wa Kimbugu Muleba Temmy Alfonce.
 Kocha wa Kagera Abdallah King Kibadeni




 Benchi la wachezaji wa timu ya Yanga katika hali ya sintofahamu
 Safu imara ya Kagera Sugar ikiongozwa na goli kipa Andrew Ntalla na walinzi wake wa karibu kama Juma Nade na Kanoni Salim wanastahili pongezi.
 Hekaheka  kuelekea langoni mwa Yanga.
 Mchezaji wa Yanga Said Bahanzi aumia  vibaya baada ya kuangka mnamo dakika ya 22 kipindi cha kwanza cha mchezo.

 Bahanzi akipata matibaba kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na  Jeryson Tegete
 Jeryson Tegete akijiandaa kuingia uwanjani
Wachezaji wa Kagera Sugar wakielekea mapumziko baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
 Mgeni Waheshima ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh. Fabian Massawe akitete jambo na Kamanda wa Mkoa (RPC)Philp Kalangi.
Mtangazaji Yusuph Abed maarufu kama  DJ y , Bi Matrida wa vision Fm Radio katika tathimini ya mchezo mzima  kutoka kwa mtangazi Abdulrazak Majid wa Kasibante Fm Radio.
 Kaka Mkuu  katika Exclusive na Abdulrazak Majid.
 Said Bahanzi akiwa tahabani
 Kagera Sugar wazidi kuendeleza historia dhidi ya Yanga.
Ndg John na Issa wao ni wadau wakubwa wa Yanga.
 Jukwaa Kuu ndani ya Uwanja wa Kaitaba.
 Sehemu ya mashabiki wa Kagera Sugar Jukwaani
 Wadau wa soka na habari  kutoka Kasibante Fm Radio
 Kamisaa wa mchezo
 Waandishi wa habari
 Sehemu ya mashabiki wa soka Jukwaa la mchanganyiko
 Jukwaa la Golani a.k.a BALIMI hali ikiwa kivingine kabisa, amani na utulivu kwa sasa vinatawala, si palestina tena!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau