WATU SABA WAFARIKI KWA KULIPUKIWA NA BOMU WILAYANI KARAGWE
30.10.2012
KARAGWE
Watu saba wakazi kijiji cha
Rugarama kata ya Ihanda wilaya karagwe
wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kitu kilichosadikiwa kuwa ni bomu.
Tukio hilo limetokea October 30 mwaka huu majira ya
saa nne asubuhi katika eneo la kijiji hicho.
Jeshi la polisi wilayani humo
limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limewataja marehemu hao kuwa ni
Eladius Robert(15),Fenius Frank(miaka 3 na miezi 6),Faraja Frank(mwaka 1 na miezi
3)na wengine waliopoteza maisha kuwa ni Scatus Kamali(15),Nelson
Lphonce(14)Edger Gidion(14) na mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja
mwenye miaka (17).
Inadaiwa kuwa marehemu
walikuwa wanaokota vyuma chakavu katika eneo la kijiji hicho kwa ajili ya kuuza
kwa wafanyabiashara wanaotoka nchi jirani,ambapo pia imeelezwa kuwa watoto wanne
kati ya hao wanatoka katika familia moja.
Mmoja wa wazazi wa marehemu
Frank Robert(35) alieleza kuwa marehemu hao walikuwa wamehitimu darasa la saba
September mwaka huu, na walikuwa wakiokota vyuma chakavu kwa ajili ya kuuza.
“jana hao wanangu ambao ni
mrehemu wana kitu kama kidumu asubuhi walikuwa
wanakusanya vyuma vyao kwenda kuuza ndio ghafra nilisikia mlipuko
mkubwa”alisema Robert.
Kwa upande wake Luteni kanali
Benedict Kitenga ambaye ni mkuu wa wilaya ya kyerwa na mtaalamu wa kutegua
mabomu, amekiri vifo hivyo kusababishwa na bomu(defencive hand grunet)ambapo
amewataka wananchi kuwa na tahadhari wanapoona kitu ambacho si cha kawaida
katika maeneo yao.
Kitenga amesema wilaya za
karagwe na kyerwa ziko mpakani na nchi za Rwanda,Burundi,Uganda na kongo, hivyo
wananchi wajihadhari na wageni wanaoingia ili kulinda amani ya nchi na maisha
yao.
MWISHO
ML