Bukobawadau

HABARI MATUKIO HARUSI YA MDAU ALMASUDI DAUDA KALUMUNA NA BI SABINA NOOR ILIYOFANYIKA JUMAMOSI YA JANA TAR.3/11/2012

 Yaap!haya tena kwa wale wakina Kaka na Dada ambao eti hamna mpango wa kuoa ... !!Huu ndio mwanzo wa shughuli nzima ya harusi ya Mdau Almasud Dauda(kamala) Kalumuna na Bi Sabina Noor,unaambiwa shughuli ni watu na watu ndio hao wamesimamia shughuli hii.
Msafara mkubwa wa Magari ukikatiza mitaa mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba,huku Gari la Maharusi likiwa na 'MABODIGADI'
Baada ya msafara huu , shughuli kubwa iliendelea katika Ukumbi wa linas Night Club kwa ajili ya Party ya kuwapongeza maharusi hawa.
 Kanda kando ya fukwe za ziwa victoria kwa ajili ya picha za kumbukumbu
 Maharusi wakichukua picha za kumbukumbu katka fukwe za ziwa victoria, kulia ni Mdau Ashraf  kaka wa Bwana harusi Almasudi Dauda Kalumuna.
 Muonekano wa  maharusi wetu Almasud Dauda Kalumuna na Bi Sabina Noor na wapambe wao.
 Kaka Mkubwa wa Bwana harusi kushoto ndg Jamal(Jamco)katka picha ya pamoja na kikosi kazi cha Mabodigadi wa harusi hii ya kipekee.
 No comment!
 Maharusi wakiingia ndani na ya Victorious hotel
 Hapa ni mapokezi ya awali,hapa ngozi nyeupe imehusika.
Kwa tabasamu mawifi wa Bi Harusi katika picha ya pamoja.
 No comment!
 Maharusi wakikata utepe wa kuingia ukumbini ndani ya ukumbi wa Club Linas.

 Tukio la kukata keki
Maharusi wakiwa tayari kukata keki.
 Wadau kwa pamoja ni familia ya Mzee Kalumuna.
 Maharusi wetu wakipeleka Keki kwa Wazazi, na zoez hili limefanyika kwa wazazi wa pande zote mbili,ikiwa ni shukrani zao kwao kwa malezi.(nadhani naeleweka mpaka hapo) ..
 Muonekano wa mapambo ukumbini, hapa mdau Mama Matungwa,maharufu kama Mama Walkgard anahusika.

 Zoezi hili linaendelea kwa Mwenyekiti wa Kamati ,na wadau wengine.
 Mr Mganyizi akipokea zawadi ya Keki kama mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harusi hii.
 Dada Rehema akipokea zawadi yake ya Keki kutoka kwa maharusi
 Mdau Jamal na mkewe Bi Jamila wakipokea zawadi yao ya Keki.
 Anaonekana  Da' Passycazia  akipokea Zawadi yake ya keki kutoka kwa maharusi wetu.
 Ama kwa hakika shughuli imeenda vyema na mambo ni mengi kweli kweli.
Pichani ni Kaka wa Bwana Harusi, Mdau Faraji na mkewe. .
 'The budyguard'
 Muda wa wageni waalikwa ukumbini kupata msosi.
 Mr &Mrs Ashraf Dauda Kalumuna(Ash Production)ni kaka wa bwana Harusi.
 Bwana Harusi Almasud akimrisha  chakula mkewe Bi Sabina Noor.
 Alikadhalika  Bi Harusi akajibu kwa kumrisha chakula mmewe.
 Pembeni kulia anaonekana  Uncle Nazzir akisema safi!


 Wadau wakiendelea kupata mulo ukumbini hapo.
Wadau wakipata msosi wa nguvu kabisa.

Next Post Previous Post
Bukobawadau