Bukobawadau

KANYIGO YETU NA CAMERA YETU NA MIKAKATI YA WADAU KATIKA KUREJESHA HESHIMA YA KANYIGO!!

Camera yetu mchana wa leo Mjini Kanyigo.
Jengo la Shirika la Posta Tanzania lililopo Kanyigo
Ofisi ya  mwenyekiti wa kijiji BUGOMBE Kanyigo.
KATIKA KUPERUZI VYANZO BUKOBAWADAU TUNAKUTANA NA TANGAZO HILI LINALO WAHUSU WADAU WA KANYINGO HIVYO NI VYEMA NASI KUONYESHA USHIRIKIANO KWA KUKUFANYA UJUWE  MIKAKATI YA WADAU WA NG'AMBO.
MMOJA WA WADAU KATIKA MIKAKATI YA KUENDELEZA KANYIGO BWANA INNOCENT LUGUMAMU; FROM BOSTON; MA STATE/USA.

Wanakundi, Ili kurejesha heshima ya Kanyigo, Kashenye katika ulimwengu wa ELIMU tumeamua kuanzisha mfuko wa elimu wa Kanyigo, ambao kwa kuanzia utalenga kuinua Elimu ya Msingi. Lengo ni kuwezesha wanafunzi wasiopungua 400 (mia nne)kuc haguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari kwa mwaka, kuanzia mwaka ujao. Tofauti na sasa ampapo wanafunzi wapatao 200 pekee huchaguliwa!!! Hata hivyo nao hao huwa hawana uwezo wa kumudu kishino cha masomo ya sekondari kutokana na msingi dhaifu katika shule za msingi!!! Huishia kupata daraja 4 au 0 wanapomaliza kidato cha 4.

 Kwa kifupi tumeamua kufanya yafuatayo ili kufanikisha mfuko huu: 1. Kuiomba kila kaya katika kata zetu zote mbili kuchangia kiasi kisicho pungua Tshs 5,000/- ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2012. 2. Kuwaomba wana-Kanyigo waishio nje ya Kanyigo, kuchangia si chini ya Tshs 20,000/- kila mmoja ifikapo mwisho wa mwaka huu 2012. 3. Watakao changia kutoka nje ya Kanyigo watume michango yao; ama kwa wakala wa M-PESA 97260 (Mama Rwegasira, Kabambilo), au kwa wakala wa TIGO-PESA 08837 (IMARISHA SACCOS, Kigarama). Bila kusahau kutaja jina lako na vilevile kuonyesha KADEA EDUCATION FUND. 

4. Njia nyingine ya kuwasilisha mchango wako ni kupitia CRDB na NMB, Imarisha SACCOS accounts: 01J2055691900 - CRDB; na 3186600382 - NMB. Usisahau kuandika kwenye Pay Slip kuwa ni fedha za KADEA Education Fund. (KUMBUKA JINA LA ACCOUNT NI: IMARISHA SACCOS). 5. Mawakala hawa watatunza kumbukumbu za michango zikionyesha majina ya wachangiaji na kiasi kilichochangwa na kuziwakilisha kwa Afisa Mtendaji KADEA kila juma. 6. Michango yote itapelekwa kwenye account ya Mfuko ambayo tayari imeshafunguliwa pale Imarisha SACCOS. 7. Kila wiki majina yote ya waliochangia yatasomwa Makanisani na Misikitini kwenye Ibada, na kutundikwa kwenye Mbao za Matangazo kwa kila Kata, Kijiji, na Vyama vya Misingi. 8. Semina ya Wadau itafanyika mara mbili kila mwaka kupokea taarifa za utekelezaji na kutathimini mwenendo wa zoezi zima. 9. Lengo likiwa kukusanya angalau kiasi cha Tshs 90 million kila mwaka. Tuna matumaini makubwa kuwa kila mwana-Kanyigo popote atakapokuwa ataitikia wito huu na kuhamasika ipasavyo. Tafadhali wajulishe wana-Kanyigo wasiopungua 5 (watano) baada ya kusoma tangazo hili. Na uchange mara moja.

 KANYIGO WATU WAMESHAANZA KUCHANGA. Kwamaelezo zaidi wasiliana na: Enock Kamuzola: MWENYEKITI KADEA - 0713333596 Michael Njumba: M/MWENYEKITI KDEA - 0784457444 Godfrey Kamukala: KATIBU KADEA - 0754366710 Moses Kagya: M/HAZINA KADEA - 0754266249 Photo: Hello wanakundi, Ili kurejesha heshima ya Kanyigo, Kashenye katika ulimwengu wa ELIMU tumeamua kuanzisha mfuko wa elimu wa Kanyigo, ambao kwa kuanzia utalenga kuinua Elimu ya Msingi. Lengo ni kuwezesha wanafunzi wasiopungua 400 (mia nne)kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari kwa mwaka, kuanzia mwaka ujao. Tofauti na sasa ampapo wanafunzi wapatao 200 pekee huchaguliwa!!! Hata hivyo nao hao huwa hawana uwezo wa kumudu kishino cha masomo ya sekondari kutokana na msingi dhaifu katika shule za msingi!!! Huishia kupata daraja 4 au 0 wanapomaliza kidato cha 4. Kwa kifupi tumeamua kufanya yafuatayo ili kufanikisha mfuko huu: 1. Kuiomba kila kaya katika kata zetu zote mbili kuchangia kiasi kisicho pungua Tshs 5,000/- ifikapo mwishoni mwa mwaka huu 2012. 2. 

Kuwaomba wana-Kanyigo waishio nje ya Kanyigo, kuchangia si chini ya Tshs 20,000/- kila mmoja ifikapo mwisho wa mwaka huu 2012. 3. Watakao changia kutoka nje ya Kanyigo watume michango yao; ama kwa wakala wa M-PESA 97260 (Mama Rwegasira, Kabambilo), au kwa wakala wa TIGO-PESA 08837 (IMARISHA SACCOS, Kigarama). Bila kusahau kutaja jina lako na vilevile kuonyesha KADEA EDUCATION FUND. 4. Njia nyingine ya kuwasilisha mchango wako ni kupitia CRDB na NMB, Imarisha SACCOS accounts: 01J2055691900 - CRDB; na 3186600382 - NMB. Usisahau kuandika kwenye Pay Slip kuwa ni fedha za KADEA Education Fund. (KUMBUKA JINA LA ACCOUNT NI: IMARISHA SACCOS). 5. Mawakala hawa watatunza kumbukumbu za michango zikionyesha majina ya wachangiaji na kiasi kilichochangwa na kuziwakilisha kwa Afisa Mtendaji KADEA kila juma. 6. Michango yote itapelekwa kwenye account ya Mfuko ambayo tayari imeshafunguliwa pale Imarisha SACCOS. 7.

 Kila wiki majina yote ya waliochangia yatasomwa Makanisani na Misikitini kwenye Ibada, na kutundikwa kwenye Mbao za Matangazo kwa kila Kata, Kijiji, na Vyama vya Misingi. 8. Semina ya Wadau itafanyika mara mbili kila mwaka kupokea taarifa za utekelezaji na kutathimini mwenendo wa zoezi zima. 9. Lengo likiwa kukusanya angalau kiasi cha Tshs 90 million kila mwaka. Tuna matumaini makubwa kuwa kila mwana-Kanyigo popote atakapokuwa ataitikia wito huu na kuhamasika ipasavyo. Tafadhali wajulishe wana-Kanyigo wasiopungua 5 (watano) baada ya kusoma tangazo hili. Na uchange mara moja.


 KANYIGO WATU WAMESHAANZA KUCHANGA. Kwamaelezo zaidi wasiliana na: Enock Kamuzola: MWENYEKITI KADEA - 0713333596 Michael Njumba: M/MWENYEKITI KDEA - 0784457444 Godfrey Kamukala: KATIBU KADEA - 0754366710 Moses Kagya: M/HAZINA KADEA - 0754266249
 Pitapita za Bukobawadau Blog katika baadhi ya shule zilizopo Kanyigo.
 Muonekano wa shule ya Msingi Kanyigo.
Mchana wa leo majira ya Saa 9 huu ndio muonekano wa Majengo Shule ya Msingi Kanyigo
 Makazi ya Mdau pande hizi.
Moja kwa moja Camera yetu ikaangaza katika Shule ya Kanyigo Muslim Seminary
 Ni wanafunzi wa kidato cha pili wa Kanyigo Muslim Seminary wakiendelea na Mitihani yao hii leo.

 Ni kupitia bukobawadau blog  kwa habari matukio ya ukanda huu, Hivyo tunaendelea kukuomba mdau msomaji kumjulisha na mwingine juu ya uwepo wa libeneke hili.
Wanafunzi wa Vidato vingine kama walivyokutwa na Camera yetu hii leo
 Sehemu ya Ibada kwa wanafunzi wa Semnary hii ya Kiislam
Madhari ya Vijiji vya Jirani na Kanyigo 
 Kama bango linavyojieleza, Mdau tunakukumbusha kupitia Older post kupata habari za muda mchache uliopita, na habari zetu kiujumla ni rukhsa kushare kwa mwenzako.
 Kivutio kikubwa katika Shule hii ni hali ya usafi wa mazingira hakika uongozi unastahili pongezi.
MWISHO
Next Post Previous Post
Bukobawadau