Bukobawadau

KUKWEPA KODI NI AIBU NA SI UJASIRI ASEMA KATIBU TAWALA WA MKOA WA MARA CLEMENT LUJAJI KATIKA SIKU YA MLIPA KODI MUSOMA


 Mgeni rasmi katibu tawala wa mkoa wa mara  clement lujaji akithubia 
meneja wa tra mkoa wa mara aliyesimama joseph kalinga akitoa taarifa ya ukusanyaji mapato kwa mgeni rasmi


wafanyabiashara wameonywa Kukwepa kodi  kwani ni aibu na sio ujasiri  walipe kodi kwa maendeleo ya taifa bila kodi taifa haiwezi kuendeshwa.

Hayo aliyasema leo wakati wa akihitimisha kilele cha siku ya mlipakodi mkoa wa mara ,sherehe hizo zilifanyika  katika uwanja wa mkendo ulioko manispaa ya musoma 

katibu tawala wa mkoa wa mara clement lujaji  alisema kuwa dhana ya ulipaji kodi kwa hiari inalenga uelewa wa mlipaji kodi yeye mwenywe na maendeleo ya taifa na jamii nzima ambapo amesema kuwa  kukwepa kodi ni aibu  na sio ujasiri
aidha  , aliwataka mamlaka ya mapato kupanua eneo la hamasa kuanzia ngazi ya kata  kwa kuwashirikisha madiwani ili kuongeza walipa kodi, kauli mbiu ulipaji kodi kwa hiari kwa mafanikio ya taifa.

;;walipa kodi ni sisi tukilipa  kodi tutaona  zahanati zinajengwa ,shule, tra panueni  mtandao   kutolipa kodi ni aibu na sio ujasiri alisema lujaji


Awali  akitoa taarifa ya ukusanyaji mapato kwa mgeni rasmi  meneja wa  Tra  mkoa wa mara joseph kalinga  alisema kuwa Mamlaka ya mapato ya mkoa wa mara imevuka  malengo  kwa kukusanya  kiasi cha shilingi bilioni 23. na kuvuka  lengo lililokusudiwa  la shilingi bilioni 22.2 kwa kipindi cha julai hadi oktoba 2012. Kalinga amesema kuwa ili kufanikisha utoaji wa huduma  yenye  ubora wa hali ya juu nay a kuvutia  kwa mlipakodi  , idara ya huduma  na elimu  kwa mlipa kodi ,imekuwa  ikitoa semina mbalimbali zenye lengo la kuwaelimisha  walipa kodi sheria  za kodi ,haki za mlipa kodi,wajibu wa mlipa kodi na wajibu wa mamlaka ya mapato imeongeza ushirikiano  baina ya walipa kodi  na watoza  kodi  pamoja  na kuinua  kiwango cha ulipaji  kodi kwa hiari.

Meneja amesema kuwa hali ya makusanyo  kwa mwaka wa fedha wa 2011/12,mkoa wa Mara ni sawa na asilimia 86 ya lengo lililowekwa hapo awali la kukusanya shilingi bilioni 63.5 kwa kuwa mamlaka imefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 54.7

Aidha  kalinga ameelezea changamoto zinazowakabili ni pamoja ongezeko la mahitaji ya mapato  ya serikali katika kutekeleza  mikakati  yake  ya kupambana na umasikini ,ukwepaji kodi kwa kupitia  njia zisizo  rasmi  wakati wa kuingiza bidhaa nchini  au kutoa bidhaa kwenda nje ya nchi,ukwepaji kodi  kwa njia ya kutotoa risti sambamba na matumizi hafifu ya mashine  za kutolea  risti  EFD) kwa wasiosajiliwa katika kodi ya ongezeko  la thamani  VAT.

Mamlaka kwa kushirikiana  na vyombo vingine  vya uthibiti  ambavyo ni jeshi la polisi ,usalama wa taifa na uhamiaji vimeweka  mkakati  wa kukabiliana na changamoto  inayohusu  ukwepaji kodi  kwa kutumia njia mbalimbali.

Naye mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa mara bartazar dibogo amewataka mamlaka ya mapato kujenga mahusiano mazuri na walipa kodi  na kamwe wasikubali  kupewa rushwa na wafanyabiashara  wapunguziwe makadirio ya mapato .Kauli mbiu  ulipaji kodi kwa hiari kwa mafanikio ya taifa


Na Pascal Michael Buyaga
Musoma
Next Post Previous Post
Bukobawadau