MKUU WA MKOA AKABIDHI MSAADA WA BAISKELI KWA WALEMAVU WAWILI – KAGERA
Mkuu wa Mkoa wa Kagera alikabidhi msaada wa Baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu wawili Bw. Simon Rudovick kutoka Kamachumu Muleba na Bi Sikudhani Ibrahim kutoka Kashai Manispaa ya Bukoba.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi baiskeli za walemavu ilifanyika jana tarehe 21/11/2012 katika ukumbi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera. Aidha
Mwenyekiti wa chama cha walemavu Kagera CHAWATA alimweleza Mkuu wa Mkoa
kuwasaidia walemavu katika kufufua na
kufunguliwa tena chuo cha Walemavu Migara Izimbya.
Chuo hicho kilianzishwa mwaka
1998 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu kujifunza ufundi pia na kuwahudumia
watoto wasiokuwa walemavu. Chuo hicho kilianzishwa kwa msaada wa wafadhili toka
Swiden ambapo walitoa vifaa na kusimamia ujenzi lakini baada ya wafadhili haokumaliza
muda wao na kuondoka chuo hicho kilifungwa mwaka 2009.
Mkuu wa mkoa alihaidi
kulishughulikia tatizo hilo na kumwagiza Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Bw. Charles
Mafwimbo kuhakikisha Halmashauri za Wilaya zote mkoa wa Kagera zinatenga fungu la kuendeleza chuo hicho na
mwakani kianza tena kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha Mhe. Massawe ametoa mwito kwa Taasisi na
mashirika pia na watu binafsi kuwa na moyo kama wa Kampuni ya KUGIS waliotoa
baiskeli mbili za walemavu zenye thamani ya shilingi laki sita ili kutoa
misaada kama hiyo kwa walemavu. Pia amewataka walemavu kujihimu kufanya kazi na
kujipatia kipato na kuacha tabia ya kuombaomba ili kujikwamua kimaisha badala
ya kutegemea kuomba kila kukicha