TANGAZO LA UGAWAJI WA VIWANJA AWAMU YA TATU KWA WALIOOMBA VIWANJA MANISPAA YA BUKOBA KATIKA MAENEO YA IHUNGO, RWOME, RWAZI, MUGEZA NA IJUGANYONDO
Wote
waliopata viwanja kwenye maeneo tajwa wanaombwa kuzingatia mambo muhimu
yafuatayo:
I. Kukamilisha malipo ya kiwanja alichopata kupitia matawi
ya Benki ya Posta:
Waliopata
viwanja watembelee tawi lolote jirani la Benki ya Posta Tanzania kukamilisha
malipo ya kiwanja (yaani Gharama halisi ya kiwanja kutoa gharama ya dhamana
iliyowekwa wakati wa kuomba kiwanja).
NB: Ikumbukwe
bei ya kiwanja inauzwa kwa mita ya mraba kama ifuatavyo:
ENEO
|
MATUMIZI
|
BEI
KWA MITA YA MRABA,Tshs
|
Rwome, Rwazi, Mugeza na Ijuganyondo
|
Makazi
na maeneo ya kuabudia
|
3,000
|
Biashara na Taasisi
|
3,300
|
|
Ihungo
|
Makazi na maeneo ya kuabudia
|
3,400
|
|
Biashara na Taasisi
|
3,600
|
Kwa
mfano, malipo ya kiwanja cha makazi cha Rwome, Rwazi, Mugeza na Ijuganyondo chenye
ukubwa wa 500m2 gharama inakokotolewa kama
ifuatavyo:-
(500m2 x
3,000) – Dhamana. Kwa hiyo gharama yake itakuwa ni
1,500,000-200,000
= Tshs.1, 300,000
II. Muda
wa kukamilisha malipo:
Kila aliyepewa kiwanja atapaswa
kufanya malipo haya katika benki ya Posta kuanzia tarehe 01 Novemba, 2012 hadi
30 Novemba, 2012.
NB:
Taarifa ya malipo (kwa atakayehitaji ufafanuzi zaidi) inapatikana katika matawi
ya Benki ya Posta au Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kupitia simu
0689469965
III. Stakabadhi ya malipo kutolewa na Benki ya Posta:
Baada ya kukamilisha malipo, tawi husika la Benki ya Posta litawajibika
kutoa stakabadhi ya malipo yenye mhuri wa Benki ya Posta.
IV. Kuoneshwa viwanja kwa waliopata viwanja:
Kwa wale
waliofanikiwa kupata viwanja na kama watapenda kuoneshwa viwanja vyao,
watapaswa kufika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Idara ya Mipango Miji kwa
ajili ya kuoneshwa maeneo yao baada ya kukamilisha malipo.
Ratiba ya
kuoneshwa inapatikana Idara ya Mipango Miji na Ardhi Manispaa ya Bukoba.
V. Orodha ya watakaopata/watakaogawiwa viwanja awamu ya nne:
Zoezi la
uchambuzi wa maombi mengine yaliyosalia kwa maeneo yote au pokelewa hadi tarehe 31 Octoba,2012
linaendelea. Orodha hii itatolewa kabla
ya tarehe 30 Novemba 2012.
VI. Waliopata viwanja kwenye maeneo ya chaguo la pili:
Kutokana na kuwa
na waombaji wengi wa viwanja kwenye baadhi ya maeneo, baadhi ya waombaji
imelazimika kuwapeleka katika maeneo ya chaguo lao la pili au la tatu kama walivyobainisha katika fomu za maombi ya
viwanja.
VII. Maandalizi ya Hati miliki ya kiwanja:
Hati miliki ya kiwanja itaandaliwa
kwa wale ambao wamekamilisha malipo ya kiwanja. Mara baada ya kukamilisha malipo
ya kiwanja, kila aliyepata kiwanja atapaswa kujaza tena majina yake kikamilifu,
anwani na saini yake vitakavyotumika kuandaa hati miliki ya kiwanja. Taarifa
hizi zitajazwa kwenye fomu inayopatikana benki ya Posta ambapo malipo
yamefanyika.
Kama picha itatofautiana
na ile iliyopo kwenye fomu ya maombi ya kiwanja, aliyepata kiwanja atapaswa
kufika ofisi za Manispaa ya Bukoba kutoa uthibitisho wa mabadiliko hayo.
VIII. Orodha ya waliopata viwanja katika maeneo tajwa hapo juu
ni kama ifuatavyo:
Namba
ya fomu
|
Jina
la mwombaji
|
Eneo
alilopata kiwanja
|
Kitalu
(Block No)
|
Namba
ya kiwanja
|
Ukubwa
wa eneo
|
|
|
|
|
|
|
Orodha imetayarishwa kwa kufuata alphabeti za majina.
|
Tangazo
hili linapatikana kwenye tovuti ya UTT Tanzania na ya Mkoa wa Kagera pamoja na
mtandao wa jamii wa Bukobawadau.
Muhimu:
- Wale wote waliopata viwanja katika awamu ya kwanza na ya pili yaani kwa maeneo ya Kagondo, Nyanga, Kyasha, Buhembe, Nshambya na Makongo muda wa kufanya malipo umeongezwa hadi tarehe 30 Novemba 2012 kutokana na maombi mengi ya waliopata viwanja.
- Wale watakaoshindwa kulipa kwa muda huo ulioongezwa Halmashauri itakuwa na hiari ya kugawa viwanja kwa watu wengine bila ya taarifa nyingine.
Karibu
tuijenge upya Bukoba.
Hamisi Kaputa
MKURUGENZI WA MANISPAA
BUKOBA