WALEMAVU KAGERA WAHAIDIWA KUTAFUTIWA MIKOPO ILI KUPATA MITAJI YA SHUGHULI ZAO
Mkuu wa Mkoa Akiongea na Baadhi ya Wanakikundi wa BUDAP katika Ofisi yao Nyamkazi Bukoba
WALEMAVU
KAGERA WAHAIDIWA KUTAFUTIWA MIKOPO ILI KUPATA MITAJI YA SHUGHULI ZAO
Katika kusistiza kauli yake kwa
vitendo juu wa walemavu katika mkoa wa Kagera kujitegemea na kujishughulisha
pia kufanya kazi mbalimbali za kujipatia
kipato na kuacha kuombaomba mitaani Mkuu wa Mkoa wa Kagera ametembelea kikundi
cha Walemavu (BUDAP) Nyamkazi katika mji wa Bukoba ili kujionea jinsi kikundi
hicho kinavyojishughulisha.
Kikundi cha BUDAP ni kikundi cha
walemavu ambao wanaendesha shughuli zao za kutengeneza bidhaa mbalimbali za
mikono na kujipatia kipato kwa kuuza bidhaa hizo hasa kwa wageni mbalimbali
wanaofika hapa mkoani katika sekta ya utalii. Bidhaa hizo ni ngoma za asili,
vidani mbalimbali pamoja na bidhaa nyinginezo mbalimbali za mikono.
Baada ya Mhe. Massawe kufika
katika kituo hicho na kujionea jinsi kikundi hicho kinavyojishughulisha na kazi
za mikono amehaidi kuwatafutia mtaalam wa kutengeneza andiko la mradi ili afike
katika kituo hicho na kuwatengenezea andiko ambalo atalitumia kuwatafutia
wafadhili ili waweze kupata mikopo kupitia andiko hilo.
Pia amewasistiza walemavu hao kubuni
miradi zaidi itakayowavutia wafadhili katika kuwasaidia. Vile vile Mhe. Massawe
amewahaidi kuwa ataongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ili
naye awatembelee na kuona shughuli zao na jinsi ya kuwakwamua katika kupata
mtaji wa kujishulisha zaidi.
Changamoto kubwa walionayo
walemavu hao ni wenzao kuwakimbia na kutopenda kujishughulisha na kuishia
mijini na kuendelea kuombaomba ambapo wanasema kuwa walianza kikundi na watu 20
lakini mpaka sasa wamebakia wanawake wawili na wanaume watano tu.
Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera
alitoa kauli ya walemavua kuacha kuwa wategezi wa kuombaomba barabarani na
mijini na kutafuta miradi ya kujishulisha ili wajipatie kipato cha kujiinua wao
wenyewe na familia zao waka, kauli hiyo aliitoa wiki jana Alhamisi tarehe
22/11/2012 wakati akikabidhi msaada wa baiskeli mbili kwa walemavu.
Na; Sylvester
Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012