WAZEE WA KIZIBO EXTRA BONGO WAFUNIKA MBAYA MJINI GEITA USIKU WA JANA SASA NI ZAMU YA BUKOBA HII LEO 7/11/2012 KATIKA UKUMBI WA BUKOBA CLUB CHINI YA UDHAMINI MKUBWA WA WINDHOEK BIA
Kiongozi wa Extra Bongo Ally Choki aka Mzee wa Farasi akizikonga nyoyo za mashabiki wake ndani ya ukumbi wa Desire Mjini Geita Usiku wa kuamkia leo katika show ya Uzinduzi wa Bia ya Windhoek chini ya Udhamini mkubwa wa Kampuni ya Mabibo Bia.
MWANAMUZIKI wa Bendi ya Extra Bongo 'Wazee wa Kizigo', Ramadhan Masanja 'Banza Stone atahusika na nyimbo zake hii leo ndani ya Bukoba Club.
Ndg Mdau kama kuna muimbaji katika safu ya Extra Bongo mwenye uwezo wa kipekee, basi msanii Rama aka Pentagon pichani ni miongoni wa kali, jamaa anauwezo mkubwa usipime!
Rapper mahili wa Extra Bongo, hapa BK anajulikana kama 'katanyama' kitambo alianzia Kakau Band ya Mjini Bukoba kwa nyuma anaonekana namba # 1 Tanzanian danncer 'Super nyamwela'
Mkali katika tasnia hii ya muziki wa band anajulikana kama Khadja KIMOBITEL.
Robart Katapila.
Safu ya wanenguaji wa kike yupo Happy, Kissa Whate, Janeth, Vello na Laity.
Wanaume wa Extra Bongo jukwaani.
Burudani hii imeletwa kwako na Kampuni ya Mabibo Beer, Wines& spirits Ltd wasambazaji wa Windhoek na Climax
Anaitwa Rama Pentagon
Chezea Mgodi wewe!!!!
Unaweza kuplay video hapo juu ili kuona na kusikia kinacho endelea.
Kama umeweza kushuhudia show yoyote ya Wazee wa Kizibo, basi utakubaliana nami kua jamaa wanatisha si kawaida kuanzia safu ya uimbaji hadi uchezaji
Mzee James Lugemalira kushoto ambaye ni Mkurugenzi wa Mabibo Bia , Ally Choki kiongozi wa Extra Bongo, Ndg Kamalamshauri wa kampuni na wa mwisho ni Mdau Daudi.
Wadau mbalimbali wakiendeleza maisha na Windhoek
Mambo yakizidi kupamba moto, Uzinduzi wa Windhoek kandaya ziwa, na mzuka huu utaendelea tena kwa wakazi wa Bukoba na vitongojivyake, alhamisi ijayo wapo Geita tena na Ijumaa timu nzima ya Mabibo Bia na Extra Bongo watauvamia mji wa Kahama.
Mashabiki wa Extra Bongo ndani ya Geita
Mashabiki wakizidi kupagawa na sebene la Extra Bongo.
Kila mjanja anatumia Windhoek.
Wadau wa Windhoek pichani kama anavyo onekana Dj Pembe.
Ally Choki akifurahi na Climax kinyaji kinacho sambazwa na Kampuni ya Mabibo Bia
Wadau na mashabiki Mjini Geita wakifurahia show
Mkurugenzi wa Desire Ndg Simon akicheck na camera yetu
Wanenguaji wa Extra Bongo wakizidi kuwajibika
Sebene la Extra likiendelea kunoga.
Furaha inapokolea.
.Mashabiki Mjini Geita.