Bukobawadau

ONYESHO LA MWANAMUZIKI KOFII ILOMODE UWANJA WA KIRUMBA JIJINI MWANZA

Mambo makubwa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba usiku huu  jijini Mwanza ambapo Mwanamuziki Gwiji Barani Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kofii Olomide amepagawisha mashabiki wa muziki wake, katika tamasha la Tusker Carnival  na kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki  jijini humo, Mwanamuziki Kofii Olomide akiwa na kundi lake amefanya kilichokuwa kikitarajiwa pamoja na hamu ya mashabiki kupiga kelele kwa madai ya kutaka kumuona mwanamuziki huyo mahiri barani Afrika.
 Cindy katikati Mwimbaji mahili wa mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani kalba ya Kofii kupanda jukwaani.
 Shughuli iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao wakicheza kwa sataili ya aina yake.
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide.
Jukwaani ni Recho wa kundi la  THT kutoka jijini Dar es salaam akinendelea kutoa burudani jukwaani
Waimbaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakiimba kwa hisia katika enesho hilo 
 Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho hilo.
Wasanii wa Kundi la THT likitumbuiza katika onesho hilo.
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe kabisa kutoka kwa wanenguaji wa Kofii Olomide.
 Kofii akiwa na mwimbaji wake anayejulikana kwa jina la Cindy akimtambulisha kwa mashabiki wa jijini Mwanza .
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe kabisa kutoka kwa wanenguaji wa Kofii Olomide.
 Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku wakiwa wameshikana.
`
 Ili mradi burudani iliyopangika kutoka kwa wanenguaji hao PICHA KWA HISANI YA FULL SHANGWE BLOG
Next Post Previous Post
Bukobawadau