Bukobawadau

RAIS MUSEVEN WA UGANDA ATAKA MAISHA YA WANANCHI WA MKOA WA KAGERA YABOREKE KUPITIA UFUGAJI WA KISASA

 Daktari Mshauri Mwandamizi Mambo ya Mifugo Ikulu ya Rais Museven Daktari Sam Byagagaire Akionyesha Ng'ombe Waliozalia Njiani Mara Baada ya Kuwasili Mtukula, Akiwa na Professa Anna Tibaijuka na Mkuu wa Mkoa
 Daktari Sam toka Uganda,Professa Anna, na Mkuu wa Mkoa wakionyesha Ishara ya Kupokea Ng'ombe 100 na Ndama watatu toka Uganda
Profesa Anna Akionyeshwa Sehemu ya Ng'ombe kunywea Maji Katika Chuo cha Kilimo Maruku Ng'ombe hao Walipofikia na Watakapotunzwa.


Wananchi wa Mkoa wa Kagera na Tanzania kwaujumla wamepokea zawadi ya ng’ombe 100 kutoka kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganada kwa ajili ya kuwaondolea umasikini na kuinua kipato cha maisha kwa kufuga na kuzingatia ufugaji bora na wenye tija hasa kwa mwananchi wa Kagera.
Ng’ombe hao (Nkole 50 na Frijeni 50) walipokelewa na Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Profesa Anna Tibaijuka pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe katika eneo la Mtukula Wilayani Missenyi kati ya mpaka wa Uganda na Tanzania tarehe 20/12/2012 siku ya Alhamisi.
Rais Museveni  alitoa zawadi hiyo kwa  Watanzania baada ya Profesa Anna Tibaijuka na Mhe. Massawe kuongoza kikundi cha Wakulima na Wafugaji kutoka mkoani Kagera kwenda nchini Uganda  na kufanya ziara ya mafunzo kuhusu ufugaji na kilimo cha kisasa mwishoni mwa mwaka jana 2011.
Baada ya Rais Museven kuwapokea wakulima hao na kuwaonyesha jinsi wananchi wake walivyonufaika na ufugaji wa kisasa pia kilimo cha kisasa alihaidi kuwa angetoa ng’ombe mia moja kwa ajili ya wakulima hao ili wakajifunze kwa vitendo na kufuga ufugaji wa kisasa.
Ng’ombe hoa waliwasili mpakani mtukula chini ya uangalizi mkubwa wa Daktari Mshauri Mwandamizi Mambo ya Mifugo Ikulu nchini Uganda, Daktari Sam Byagagaire. Jambo la kushangaza na kustaajabisha kati ya Ngo’mbe hao mia moja watatu walizalia njiani na kufikisha idadi ya jumla ya 103.
Baada ya kupokelewa mifugo hao walipelekwa katika kituo cha kilimo cha Maruku ambapo watakuwa wanatunzwa hapo na kutumika kwa mafunzo ambapo Mkuu wa Chuo hicho Daktari Jackson Nkuba alisema hiyo ni nafasi nzuri ya wanafunzi wake kujifunza kwa vitendo kwani hapo awali walikuwa na ng’ombe wanne tu pia na kufanya utafiti halisi wa mifugo kupitia ng’ombe hao.
Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kagera alitoa shukrani zake kwa Rais Museven kwa kutoa zawadi hiyo  ambapo alisema kuwa nchi za Tanzania na Uganda zinashirikiana na zina mahusihano mazuri  na kuwaomba wananchi kuchukua nafasi hiyo kujifunza ufugaji bora ili kuinua hali zao kupitia fursa hiyo ya zawadi ya ng’ombe 100.
Na;         Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012
Next Post Previous Post
Bukobawadau