Bukobawadau

RAYC Amshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu

 RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa matibabu ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.Rehema aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi RayC Bibi Margareth Mtweve(kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C(Picha na Freddy Maro)
Next Post Previous Post
Bukobawadau