Bukobawadau

VURUGU KUBWA ZIKIENDELEA KASHAI WANANCHI WACHARUKA KUMUAMISHA MTUHUMIWA TUKIO LIMEGUBIKWA NA UTATA UTARATIBU WA KULISEMEA HAUPO.!!

 Polisi wakiendelea kudhibiti vurugu kubwa zinazoendelea kufuatia  tukio lililotokea usiku wa jana baada ya Wananchi kumhusisha Mwalimu Bernadeta Katabalo wa Kashai shule ya msingi kwa kile kinacho semekana kuwachukua watoto Msukule, ingawaje habari zilizopo ni kwamba Watoto ni wa Mdogo wake aliyekuwepo nyumbani hapo na wanae baada ya kutoka Msibani uko kijijini Bushagala Kamachumu kufuatia kifo cha mmewe kanali Bukende(hadi uvumi huu unaanza)
 Vijana wa Kashai wakiendeleza Mtiti kwa kuwarushia mawe Polisi.
 Baadhi ya Raia wakiwa mikononi mwa Polisi kufuatia kuhusishwa na Vurugu hizi.
 Pamoja na kupigwa mabomu ya machozi , wananchii wanaonyesha kuvumilia kwa kunawa maji usoni .
Shughuli hii imefanywa kiroho safi na walimu wenzake wa Shule ya msingi Kashai.
Hivi ndivyo Camera yetu ilivyo weza kupenyeza.
 Sehemu ya wanahabari wakipata maelezo juu ya tukio hili ambapo chanzo ni baada ya Mama mmoja mdogo wake Mama Malikia au Mwalimu Bernadeta ajulikanae kwa jina la Benedicta Bukende ambaye ni Mjane kufuatia kifo cha mmewe aliyekuwa( Kanali) kilichotokea hivi karibuni jijini Dar es salaam na mazishi kufanya Ijumaa iliyopita nyumbani kwao  kijiji kamachumu.

Sakata lilianza pale tu ndugu wa Marehemu walipokuja mjini nyumbani kwa Mwalimu Bernadeta kwa lengo la kumtaka Mjane na watoto wake wawili warudi kijijini ili wakamilishe hata siku za Novena kutokana na taratibu za kidini, yakatokea majibishano ya pande mbili licha ya kwamba Mjane na watoto walitekeleza kile kilichoamuliwa na ndugu wa Marehemu na kurudi kijijini.
 Kulia ni Mzee Ruobya ambaye ndie mwenyekiti wa Mtaa huu wa Majengo ,akifanya yake katika kusimamia Mali za Mama mwenye Nyumba Mama Malick au Mwalimu Bernadeta Katabalo aliyepata dhahama ya kutuhimiwa kutokana na Majibishana na mawifi wa Mdogo wake Bi  Benedicta Bukende kwa kile walichodai hakuwa na lengo zuri kumshawishi  mdogo wake huyo kutoka msibani  na watoto mapema.Mpaka sasa swala hilo lipo polisi na Raia wanacharuka kwa sababu hawana ufafanuzi juu ya swala hili.

BUKOBAWADAU BLOG TUNAKUJUZA  KILE KINACHOENDELEA NA HATUNA JIBU LA UKWELI  JUU YA  YANAYO ONGELEWA!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau