WANAKAMATI WA HARUSI YA MDAU PATRICK POMBE MAFISANGO WAHITIMISHA RASMI KAZI WALIOPEWA
Muonekao wa wanakamati waliojitokeza katika ukumbi wa Fiosmimi Hotel kushiriki kikamilifu katika hitimisho la shughuli waliyopewa.Kabla ya yote mdau nakupa picha kadhaa za Wawili hawa katika pozy, na mikato mbalimbali,nikagundua kuna mengi hatukuyajua kuhusiana na Mdau Patrick Pombe.
Ni shughuli ya kuhitimisha rasmi kamati ya harusi ya wawili hawa pichani ambapo mambo mengi yamejitokeza, yakuvutia na yakujifunza kwa namna moja hama nyingine.
Jambo jingine usilolijua kuhusu Patrick aka Mafisango,nimegundua wawapo matembezini muda mwingi wanashikana mikono kuonyesha mshikamano.
Mikato ya ziada kama hivi.
Busara ni kitu kingine walichonacho wawili hawa na hii ni kutokana na maelezo yao pale walipopewa fulsa ya kutoa shukraniWakati Mdau Patrick anamtambulisha mkewe kwa Wanakamati
Kauli mbiu kutoka kwa Patrick kuwa Maisha ni matamu unapokua na mwenzako,anajilaumu kuchelewa
Nidhamu ya hali ya juu kimatendo na kimtazamo tu
Naam hakika wamependeza na wanarandana
Kaka Mkuu akitoa angalizo.Kaka mkubwa akifunguka muda mchache kabla ya sala ya chakula.
Sala fupi ya chakula ikiongozwa na Bi harusi wetu Bi Beatrice.
Wadau katika unyenyekevu.
Kwa heshima ,wakitangulia wawili hawa.
Kuna wauzaji wa chakula, na waandaaji wa chakula pia wapo wasambazaji, hapa namuongelea Bi Hawa Maburuki mwanamama wa Kimanyema ,wengi wanamjua kama Mama Hassan kichwabuta binafsi nimemzoea kwa jina la Mama Matola au Mama Husna huyo ndo mkali wa mapishi kama si kanda ya ziwa basi utakuwa na yako wewe!!huyo ndo muandaaji na mpishi wa Menu yetu kwa usiku huu.
Rafiki yangu Mmoja na rafiki wa Kaka Mkubwa ajulikanae kwa jina la Makusalo na ware kila siku utokea kemondo kwa ajili ya kupata chakula cha mchana kwenye Mghahawa wa HH unaomilikiwa na Bi Hawa,hakika mwanamama huyu pichani kushoto anaweza na anayamudu mapichi.
Wadau pichani ni Mr Matovelo, Ndg Jamal, Mr Self Mkude kwa pamoja na Mzee Deo Deka.
Mdau Danny akifuatiwa na Elihabu.
Mr &Mrs Makoko.
Wananzengo pichani wakipata msosi.
Wadau wakiendelea kupata chakula.
Vile mambo yalivyo sehemu nyingi ukipata msosi ni kushushia Rwenzori na kinywaji chako cha Windhoek
Salim B0NGE ambaye nae yupo mbioni hapa akitoa neno
Anaitwa Manyama akionyesha kuguswa na tukio la rafiki yake.
Mr Matovelo
Mdau Mr Ance akijaribu kufanya yake.
Wakati Kaka Mkude akitoa wosia kwa maharusi hawa, kikubwa alichokisema anadai yeye na jamaa zake Mtensa na Deo wamo kwenye ndoa zaidi ya miaka 30 na hakuna shaka kabisa.
AUDIO ya maongezi ya Mr Self Mkude itakuijia kuptia email yako Mdau msomaji
Baada ya mambo yote kamati imeweza kukabidhi kiasi kilicho salia ikiwa ni jumla ya Tsh 500,000/=
Kikubwa hapa najaribu kukumbuka kamati nyingine,na matendo yale.....Bango la Fiosmimi Hotel ilipofanyika shughuli hii ni usawa wa ziwa Victoria .
Mjengo wa Fiosmimi Hotel.