Bukobawadau

WAZIRI WA HABARI, VIJANA, MICHEZO NA UTAMADUNI DR. MUKANGARA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA.

 Katibu Tawala Mkoa Kagera Akimpokea Dr. Fenella Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
Dr. Fenella Mukangara Akisaini Kitabu cha Wageni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
 Mhe. Massawe Mkuu wa Mkoa Kagera Akisoma Taarifa ya Mkoa Kwa Dr. Fenella Mukangara
Wanahabari Wakiwajibika Mbele ya Waziri wa Wizara Inayohusika na Masuala ya Habari

Waziri wa Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni Mheshimiwa Daktari Fenella Mukangara yupo  hapa mkoani Kagera  ambapo amefika  kukagua shughuli mbalimbali zinazohusiana na  Wizara yake.  Mara baada ya kufika alipokelewa na Mkuu wa Mkoa ofisini kwake na kusomewa taari fa ya mkoa leo tarehe 27/12/2012 majira ya saa tatu na nusu asubuhi.

Dr. Mukangara pamoja na shughuli nyinginezo pia ataweza kutembelea SACCOS na vikundi mbalimbali vya ujasiliamali ili kujionea shughuli zinazofanywa na vikundi hivyo hasa hasa vikundi vya vijana.
Baadhi ya vikundi vya ujasiliamali vitakavyotembelewa na Mhe. Waziri ni pamoja na vikundi vya Ibwera SACCOS (Halmashauri ya Wilaya Bukoba) pamoja na TUMEJIARI SACCOS (Manispaa ya Bukoba). Vilevile SACCOS zenyewe zitatembelewa katika makao makuu yake.
Mhe. Dr. Mukangara katika ziara hiyo atakagua au kupewa taarifa jinsi vijana walivyonufaika na mikopo ya Rais Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mikopo hiyo inajulikana kama Mabilioni ya JK.
Aidha Mhe. Waziri wakati akipokea taarifa ya mkoa aliweza  alibainisha kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni kwa sasa inaweka mkakati wa takwimu za vijana ili kujua vijana wanafanya nini na wanajishughulisha na nini ili serikali iweze kuwawezesha kwa mikopo zaidi ili kuongeza ajira zaidi kwa vijana.
Vilevile Waziri Mukangara hakusita kuongelea juu ya vyombo vya habari yeye kama waziri mwenye dhamana  ya masuala ya habari, ambapo alisisitiza  sana juu ya radio na magazeti yaliyopo hapa mkoani kuhakikisha yanafanya kazi kwa leseni  yaani  vyombo hivyo viwe vimesajiliwa na vinafanya kazi kihalali.
Kwa upande wa redio zilizopo hapa mkoani Waziri Mukangara ametoa angalizo juu ya kuhakikisha zinafuata maadili na misingi ya utangazaji na ufikishaji wa habari kwa wananchi bila kuwaposha, kuchochea au kuhamasisha wananchi kwa masuala yasiyokuwa na tija na kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.
Na;         Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa
KAGERA @2012

Next Post Previous Post
Bukobawadau