BASI LA BUNDA LAPATA AJALI HII LEO 9.1.2013
Basi
la Bunda lililokua linatokea Musoma kwenda Mwanza limepata ajali nje
kidogo ya Magu eneo la katikati ya Kahangalala na Ihayabuyaga na watu
watatu wanahofiwa kufariki katika ajali hiyo na zaidi ya 10 kujeruhiwa.
Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao.
Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.
Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri.
Hali ya baadhi ya barabara za ndani zinazounganisha vijiji wilayani Magu zimefunikwa na maji
Baadhi ya nyumba zilizo karibu na eneo la ajali nazo zimeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili wilayani Magu.
Barabara hali ya hewa na mazingira.
Mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa na hofu kubwa imetanda eneo la tukio kuhofia usalama wa hali za abiria waliomo ndani ya basi husika kwani basi limepinduka tairi zikielekea juu, limetumbukia kwenye majaruba ya mpunga, limepondeka vibaya upande mmoja, na tayari katika muda huu napita eneo la tukio miili ya watu wawili imeonekana ikizagaa nje ya basi kandokando ya barabara na mvua kubwa inaendelea kunyesha.

PICHA KWA HISANI YA GSENGO |