Bukobawadau

BASI LA MAGU TRANS LAPINDUKA LIKIELEKEA WILAYANI NGARA

Basi la Magu Trans lenye nambari  T557AAH lapinduka muda mchache baada ya kutoka Sengerema likielekea Ngara ,hivi ndivyo lilivyikutwa na Camera yetu asubuhi ya leo.
Camera yetu katika kudadisi imegundua ama ni tatizo la tairi au mwendo wa kasi uliopelekea kuacha njia na kubinuka nje ya barabara kuu ya kutoka Jijini Mwanza kuja Mjini Bukoba kabla ya kufika Geita.
Kwa  ndani hali iko hivi.
Watu wote wamejeruhiwa ila hali ya kondakta wa basi ili ilionekana kuwa mbaya na ili kumtoa ilibidi  basi inyanyuliwe kwa jeki kama inavyo onyesha katika picha, zoezi lililofanikiwa na kumkimbiza hospital
Wengine husema kufa kufaana,wengine kwako harusi kwangu matanga,wengine husema  mgeni karibu mwenyeji apone wahaya tunasema 'BASHEKELA MBALI BYEZILE'
Busy ile mbaya kutoboa Tank la mafuta, tunajifunza nini hapo? Inawezekana kuna wenzetu uombea matukio haya yatokee ili angalau vijana wao waweze kwenda shule na yeboyebo mpya.
BUKOBAWADAU TUMEKUWA TUKIJIULIZA MASWALI BILA MAJIBU,AJALI ZA NAMNA HII NI JAMBO LA KAWAIDA HAPA NCHINI, KUDHIBITISHA ILI JARIBU KUSAFIRI KWA NJIA YA BARABARA KUTOKA MKOA MMOJA KWENDA MWINGINE MFANO BUKOBA KWENDA DAR UTAONA KAMA SIO LORI,SEMI AMA BASI LIMEACHA NJIA NA  KUPINDUKA,JE HALI HII HAIWEZI KUPATIWA  DAWA JAPO YA KUPUNGUZA MAANA KUISHA KABISA SIO RAHISI?
SEMINA KWA KWA MADEREVA NA WAMILIKI WA VYOMBO HIVI INATAKIWA MARA KWA  MARA NA SISI WASAFIRI TUWE MACHO KUKEMEA MWENDO KASI NA ULEVI KWA MADEREVA,TUMESHUHUDIA MARA KADHAA DEREVA ANAPIGA KIROBA,ANAVUTA BANGI,GOMBA ,KABASANGA  MIRUNGI,MUDA WOTE SHAVU LIMEVIMBA,PEMBENI YUPO NA DEMU WAKE ABIRIA TUNACHUKULIA POA, TUNAKAUSHA, TUNATAZAMA TU HAKIKA BUKOBA WADAU  TUNASIKITIKA SANA TUKUMBUKA HUU MWAKA UNAITWA 'WEBANGE' ABIRIA TUNAWAOMBA MSIYAFUMBIE MACHO MATENDO HAYA.!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau