CHANJO ZA NIMONIA NA KUHARISHA ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA MANISPAA YA BUKOBA
Akina Mama (Wazazi) Waliofika Katika
Kituo cha Afya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba ili Watoto wao Kuchanjwa
Chanjo za Nimonia na Kuharisha.
Akina Mama Hawa Wakitabasamu na Vichanga Vyao (Siri ya mtoto Aijuaye Mama)
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Massawe Akizindua Chanjo ya Nimonia na Kuharisha kwa Kumpa Mmojawapo wa Watoto Walioletwa Katika Uzinduzi Huo.
Mkuu wa Mkoa Akiendelea Kutoa Chanjo, Alizindua Kwa Vitendo Kwelikweli.
Mkuu wa Mkoa Akiendelea Kutoa Chanjo, Alizindua Kwa Vitendo Kwelikweli.
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe.Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe azindua rasmi chanjo ya Nimonia na Kuharisha kwa watoto chini ya miaka mitano (U 5) mkoani Kagera. Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 2/01/2013 katika Kituo cha Afya cha Rwamishenye Manispaa ya Bukoba.

Katika uzinduzi huo wa
chanjo mpya za Nimonia na Kuharisha ambazo zinatolewa kwa mara ya kwanza nchini ukiwemo
mkoa wa Kagera unaotegemea kuchanja jumla ya
watoto wapatao 109,407 kwa wilaya zote saba, takwimu hizo zilitolewa na Dk. Salum I.Sufiani
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa katika uzinduzi hizo mpya.
Aidha Mhe. Massawe kabla ya
kuzindua chanjo hizo aliwaasa wazazi (akina mama) walioleta watoto wao kwa
ajili ya kuchanjwa kuzingatia uzazi wa mpango na kuachana na tamaduni za zamani, “Kwa sababu zamani hakukuwapo na chanjo za
aina mbalimbali, wazazi walizaa watoto wengi ili wakifa, watoto wengine wabaki
lakini sasa chanjo za kuzuia vifo vya watoto zipo” Alisistiza Mkuu wa Mkoa.
Pia Mkuu wa Mkoa alisistiza
ubora wa chanjo hizo za Nimonia (Uti wa Mgongo) na kuharisha kuwa zina viwango
vinavyotakiwa na hazina madhara, zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani
(WHO). Wananchi walisistizwa kuhakikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka
mitano wanachanjwa bila kuhofia chanjo hizo.
Vilevile Mhe. Massawe
aliwaomba wazazi kuzingatia ratiba ya chanjo hizo ambapo chanjo ya kuharisha
inatakiwa mtoto apewe dozi ya kwanza ndani ya wiki 15 tu na dozi ya pili apewe
mtoto ndani ya wiki 32 tu. Aidha chanjoa ya Nimonia mtoto anatakiwa kupewa
katika wiki ya 6, wiki 10 na wiki ya 14 tu.
Kutokana na magojwa ya
kuharisha kusabibishwa na uchafu, Mkuu wa Mkoa hakusita kuwasistiza wananchi wa
Kagera kudumisha usafi katika maeneo yao hasa hasa wakina mama wenye watoto
wachanga. Pia aliwashukuru wakazi wa Manispaa ya Bukoba kwa kuuweka mji wao
katika hali ya usafi unayoridhisha.