JIJINI MWANZA BARAZA LA MADIWANI MANISPAA YA ILEMELA LAENDELEA KUKUMBWA NA MTAFARUKU KWA MADIWANI WA CHADEMA KULISUSIA.
Wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.
Naibu meya wa Manispaa ya Ilemela Bw. Dede Swila (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho ambacho kilianza na zengwe pamoja na makeke mengi lakini kiliisha kwa salama.
Afisa habari wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Bi. Viola (kushoto) akiwa na ameketi meza moja na wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.
Diwani wa kata ya Buswelu Thobias Mpemba akichangia hoja kati ya ajenda zilizo wasilishwa.
Mtaalamu wa moja kati ya vitengo wilaya ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwamoja ya hoja zilizowasilishwa.
Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata akitoa ufafanuzi ndani ya kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika leo jijini Mwanza na kuhusisha pia na wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake wa wilaya hiyo .
Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Kufuatia mtafaruku huo uliopelekea Madiwani wa
CHADEMA kutoka na kususia kwa mara nyingine kikao cha baraza, Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ananini cha kusema juu ya hali hiyo na hali
hii ya kutokukubalika na madiwani wenzake wa CHADEMA anaichukuliaje
Licha ya kusaini kitabu cha mahudhurio na kususia kikao hicho, madiwani hao wa CHADEMA baadaye walionekana wakiingia kwenye chumba cha mhasibu wa Manispaa ya Ilemela na kuchukuwa posho zao za kuhudhuria kikao hicho cha kujadili masuala ya maendeleo.
Naibu meya wa Manispaa ya Ilemela Bw. Dede Swila (CCM) akichangia hoja kwenye kikao hicho ambacho kilianza na zengwe pamoja na makeke mengi lakini kiliisha kwa salama.
Afisa habari wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela Bi. Viola (kushoto) akiwa na ameketi meza moja na wataalamu na wafanyakazi wa idara mbalimbali wakifuatilia yanayojiri ndani ya kikao hicho.
Diwani wa kata ya Buswelu Thobias Mpemba akichangia hoja kati ya ajenda zilizo wasilishwa.
Mtaalamu wa moja kati ya vitengo wilaya ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwamoja ya hoja zilizowasilishwa.
Meya wa Manispaa ya Ilemela ambaye pia ni diwani wa kata ya Kitangili, Bw. Henry Matata akitoa ufafanuzi ndani ya kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika leo jijini Mwanza na kuhusisha pia na wataalamu wa vitengo mbalimbali na idara zake wa wilaya hiyo .
Jengo la Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Na. ALBERT G. SENGO: MWANZA
BARAZA la Madiwani wa Manispaa ya Ilemela limendelea
kukumbwa na mtafaruku kwa Madiwani wa Chama cha CHADEMA Wilayani humo kuendelea
na msimamo wao wa kutomtambua Meya Bw.
Henry Matata (CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Kitangiri na kususia kikao
cha Baraza hilo kilichofanyika leo katika ukumbi wa ofisi za Mkuu wa Wilaya
hiyo eneo la Busweru jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Zubery Mbihna mara
tu alipomaliza kuwasilisha ajenda saba za kikao hicho Diwani wa Nyakato Bw.Josephat
Manyerere (CHADEMA) alinyanyuka na kutaka ajenda ya Maswali na Majibu iwe ya
kwanza kujadiliwa na Chama Chake kiwe
cha kwanza kuwasilisha maswali yake iliyokuwa imeyaandaa hali iliyoleta
mabishano makali na kelele za malumbano hali iliyopelekea Madiwani wote wa CHADEMA kutoka nje ya ukumbi.
Hata hivyo Meya Bw. Matata kwa kuzingatia taratibu,
kanuni na sheria zilizopo za Halmashauri hiyo aliwatuliza wajumbe waliosalia wakiwemo
wataalaamu kisha akatangaza kuendelea na ajenda kama zilivyo wasilishwa na
Mkurugenzi wa Manispaa hiyo ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Madiwani.