Bukobawadau

KISA NA MKASA MTAANI

Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha basi wakafanya mazungumzo. Mmoja aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia yake hatimaye mwenzake akasema " Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi sikiliza kisa changu hiki….

"Miaka michache iliyopita nilikutana na mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa tu na mimi na huyo mjane tukaamua kuoana. Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa kambo (yaani binti wa huyu mke wangu niliyemwoa akiwa mjane), hivyo huyo binti yangu wa kambo akawa mama yangu wa kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu wa kambo wa kiume ambapo mke wangu akawa mama mkwe wa mkwe wake.

Baadaye binti ya mke wangu yaani binti yangu wa kambo (ambaye kwa sasa ndiye mke wa baba yangu na hivyo kuwa pia mama yangu wa kambo) alipata mtoto wa kiume. Mtoto huyo wa kiume akawa mdogo wangu kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini kwa vile pia alikua ni mtoto wa binti wa mke wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke wangu na mimi nikawa babu yake huyo mdogo wangu.

Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume. Sasa msichana (yaani binti ya mke wangu ambaye pia ni mke wa baba yangu) ambaye ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia bibi yake na mwanangu (mwee!!). Hali hiyo ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa mtoto wangu (achilia kuwa babu yake!!) ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo (anti) wa binti yake mwenyewe . Mtoto wangu wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
Next Post Previous Post
Bukobawadau